| Messi na Maradona |
BUENOS ARIES, ARGENTINA
STAA wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Argentina, Jorge Voldano, amesema staa wa Barcelona, Lionel Messi ni mchezaji hatari lakini nyota wa zamani wa Argentina, Diego Maradona alikuwa fundi zaidi.
Messi Jumanne ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote Barcelona baada ya kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 5-3 wa Barcelona dhidi ya Granada na Voldano anaamini kwamba Messi anaweza kuwa mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea duniani.
Tunamhukumu Messi kwa maisha yake yote ya soka, wakati Messi bado ana miaka 24 tu. Ukweli kwamba mpaka sasa tumefikia hatua ya kuwalinganisha ni heshima kubwa kwa kile ambacho Messi amefanya, alisema Voldano.
Jumamosi hii Messi ana nafasi ya kuendeleza idadi yake ya mabao 234 aliyofunga mpaka sasa wakati Barcelona itakapokuwa ugenini kucheza na Mallorca wakati huu ikiifukuza Real Madrid iliyo kileleni kwa tofauti
No comments:
Post a Comment