| GEPU KWA SASA NI POINT 6 TU. REAL MADRID NA BARCELONA |
SARE mbili za Real Madrid zimefanya njia ya kusaka ubingwa katika Ligi Kuu Hispania iwe wazi.
Hiyo ni kwa kuwa tofauti kati ya Barcelona na Real Madrid kwa sasa ni pointi 6 pekee. Awali Real ilikuwa mbele kwa pointi 10 lakini imefululiza sare mbili na kujiongezea wasiwasi.
Sasa Barcelona, ambayo itacheza na Real Mallorca leo Jumamosi, imepata mwanya wa kutoa presha kubwa kwa wapinzani wao.
Kama mabingwa watetezi Barcelona wataifunga Real Mallorca,
watakuwa nyuma ya wapinzani wao kwa pointi tatu, na kama Real Madrid wakishindwa kuifunga Real Sociedad saa mbili baadaye, maana yake ni kwamba wanaweza kupoteza nafasi ya ubingwa wakati wowote.
Baada ya kushinda mechi 11 mfululizo, Real imejikuta ikitoka sare ya bao 1-1 mara mbili. Kwanza ilikuwa dhidi ya Malaga na baadaye Villarreal.
Wachezaji wa Jose Mourinho ambao wamefunga jumla ya mabao 90 katika mechi 28, wameshindwa kutakata katika mechi za karibuni na wachezaji wamechanganyikiwa kutokana na matokeo hayo.
Katika hali ya kawaida, Real Sociedad si kikwazo kikubwa, lakini kama wachezaji wa Real Madrid wakiendelea kuchanganyikiwa maana yake ni kuwa wanaweza kufungwa.
Barcelona ilitibuliwa safari wakati ilipofungwa na Osasuna mabao 3-2 mwezi uliopita, lakini wameshinda mechi sita mfululizo.
No comments:
Post a Comment