RIO FERDINAND: "VIEIRA ACHANA NA MAN UNITED BWANA"
Kwa mara ya pili katika Wiki mbili, Patrick Viera, ambae ana wadhifa maalum kwenye Klabu ya Manchester City, ameibuka na kudai Mabingwa Manchester United huwa wanapendelewa na Marefa wakicheza Uwanja wao Old Trafford.
Ferguson pia aliwaambia Man City kuwa yu tayari kupambana nao kwa vita ya aina yeyote ya kisaikolojia na Siku zote anayo majibu kwao.
Kauli ya Viera inafuatia tukio katika mechi ya Ligi Kuu England Jumatatu usiku ambalo Refa Michael Oliver aligoma kuwapa Fulham penati katika Dakika ya 89 ingawa pia Kipindi cha Kwanza pia aliwanyima Man United penati.
Katika mechi hiyo Man United walishinda bao 1-0 na kuipiku Man City na kutwaa uongozi wa Ligi wakiwa Pointi 3 mbele ya Man City.
Viera ametamka: ‘Ukicheza na Man United kwao huwa wananufaika. Ukienda kucheza na Man United, Real, Barca, au Milan siku zote ni ngumu kwa Refa kuzipinga Timu za aina hiyo! Hivyo ndivyo ilivyo! Timu ambazo hushinda siku zote hupendelewa! Na sie inabidi tushinde ili nasi tusaidiwe baadae!’
Hata hivyo wadau wanadai Man United wameshawahi kunyimwa penati nyingi na pia kuamriwa wapigiwe penati zisizo za haki na mojawapo ikiwa kwenye ile mechi ya mwanzoni mwa Msimu huu waliyopewa Newcastle na kusawazisha bao na kufanyamechi iishe 1-1.
Kauli za Viera zilimfanya Beki wa Man United Rio Ferdinand atoe posti kwenye mtandao wa Twitter: ‘Kwa nini Viera anajihusisha na Man United….kauli mbili katika Wiki na ushei…achana nasi bwana!!!’
Hadi sasa Sir Alex Ferguson hajazungumza lolote kuhusu matamshi ya Viera.
"Kwanini Vieira anaifuata fuata sana Man Utd........ Kutoa maoni mara mbili kuhusu United ndani ya wiki, inashangaza..........haaaaa bwana achana na sisi."

No comments:
Post a Comment