BUKOBA SPORTS

Friday, March 30, 2012

SIMBA YAMSIMAMISHA KWA MUDA MAFISANGO, MGOMO BARIDI WAISHA

Mafisango akiwa amebebwa na wachezaji wenzie.


Uongozi wa Simba chini ya Aden Rage umemsimamisha kwa muda usiojulikana kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango kwa utovu wa nidhamu, imeelezwa.

Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga amesema leo kwamba, Mafisango amechukuliwa hatua hiyo kwa utovu wa nidhamu, ambao umekuwa ukijirudia mara kwa mara. 

 
Wakati huo huo, mgomo wa wachezaji wa Simba kuhusu mgawo wao baada ya mechi dhidi ya ES Setif ya Algeria umeisha baada ya Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ kwenda kuwaongezea fedha wachezaji wa timu hiyo.
Simba ipo kambini Bamba Beach, Kigamboni, Dar es Salaam ikijiandaa na mechi ya Ligi Kuu dhidi ya African Lyon Jumamosi mjini Dar es Salaam.Baada ya mechi hiyo, Simba itaelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Se Setif, wakipitia Misri.

No comments:

Post a Comment