BARNABA MSANII WA BONGO FLAVA
MSANII aliyesheheni vipaji lukuki kutoka Tanzania, Barnaba Elias Barnabas, amesema kuwa ujumbe uliomo katika wimbo wake wa Magubegube, ni mzito zaidi ya jina la wimbo wenyewe.
"Magubegube ni wimbo ambao nilipanga kuwapa ujumbe wanafunzi wa shule hasa wa kike," anasema Barnabas.
"Magubegube ni wimbo ambao nilipanga kuwapa ujumbe wanafunzi wa shule hasa wa kike," anasema Barnabas.
Barnaba(kushoto) na Bebari la Kihaya Mpoki (kulia)
"Kuna wanafunzi ambao wanakwezwa na walimu wao baada ya kuwaridhisha kimapenzi, pia wapo ambao wanafelishwa makusudi hasa wanapokataa kuwaridhisha kimapenzi baadhi ya walimu wenye tabia mbovu. "Lakini pia ujumbe huo unawaendea na wale wanaopenda ovyo na wenye tabia chafu za kutembea na wake za watu.
"Nilikuwa na mengi na mengine nilishindwa kueleza ndani ya wimbo huo, lakini nina imani umeelimisha vile ipasavyo."
Mwaka huu mwanamuziki huyo alibahatika kupata tuzo ya KTMA baada ya kushirikishwa katika tuzo hizo kwa miaka mitatu mfululizo.
No comments:
Post a Comment