BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 11, 2012

BUNDESLIGA: MECHI KALI DORTMUND VS BAYERN MUNICH LEO SAA 3 USIKU

 
Kwa Miaka miwili sasa Bayern Munich hawajawahi kuwafunga Mabingwa watetezi wa Ujerumani Borussia Dortmund na leo Jumatano Saa 3 Usiku Bongo Taimu watatua Signal Iduna Park kuwavaa Mabingwa hao nyumbani kwao katika Mechi ambayo, bila shaka, itaamua Bingwa wa Bundesliga ni nani Msimu huu.

Huku Mechi zikiwa zimebaki 5 Msimu kwisha, Bayern Munich wako Pointi 3 nyuma ya vinara wa Ligi Borussia Dortmund na ushindi kwao utawafanya waifikie Pointi Borussia Dortmund lakini watakuwa kileleni kwa ubora wa tofauti ya Magoli wao wakiwa na 50 na Dortmund wana 44.
Akizungumzia Mechi hii, Mwenyekiti wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge, amesema: ‘Ni lazima tushinde maana hii itaamua Ubingwa. Sare si mbaya lakini tukishinda tutashika usukani na hatima yetu itabaki kwetu!’
Kila Timu imepata afueni kidogo baada ya Mastaa wao, Bastian Schweinsteiger wa Bayern na Mario Gotze wa Dortmund, kuripotiwa kuwa fiti na kuna kila uwezekano wakachezeshwa.
Mara ya mwisho Timu hizi kupambana ilikuwa ni Mwezi Novemba nyumbani kwa Bayern Uwanjani Allianz Arena na Bayern kunyukwa bao 1-0 kwa bao la Mario Goetze.
Msimu uliopita Bayern Munich walipigwa nje ndani  na mara ya mwisho Bayern kuifunga Dortmund ilikuwa Februari 2010 huko Allianz Arena waliposhinda 3-1.


TABLE ILIVYO KWA SASA

Rank
Club Matches W* D* L* G* GD* PTS*

1
Borussia Dortmund 29 20 6 3 66:22 +44 66 CL*
2
FC Bayern Munich 29 20 3 6 69:19 +50 63 CL*
3
FC Schalke 04 29 18 3 8 64:35 +29 57 CL*
4
Borussia Mönchengladbach 29 15 7 7 41:20 +21 52 CL* Qual.
5
VfB Stuttgart 29 12 7 10 52:39 +13 43 EL*
6
Bayer 04 Leverkusen 29 11 8 10 40:39 +1 41 EL* Qual.
7
SV Werder Bremen 29 11 8 10 42:44 -2 41 EL* Qual
8
Hannover 96 29 10 11 8 37:42 -5 41

9
VfL Wolfsburg 29 12 4 13 41:52 -11 40

10
1899 Hoffenheim 29 9 10 10 34:40 -6 37

11
1. FSV Mainz 05 29 8 9 12 43:48 -5 33

12
1. FC Nuremberg 29 9 5 15 27:41 -14 32

13
SC Freiburg 29 8 8 13 39:55 -16 32

14
Hamburger SV 29 7 10 12 33:51 -18 31

15
FC Augsburg 29 6 12 11 31:44 -13 30

16
1. FC Köln 29 8 5 16 36:59 -23 29 Play-offs
17
Hertha BSC Berlin 29 6 9 14 30:52 -22 27 Relegation
18
1. FC Kaiserslautern 29 3 11 15 18:41 -23 20 Relegation

No comments:

Post a Comment