BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 18, 2012

DARAJANI KUWAKA MOTO LEO, CHELSEA NA BARCELONA

Listen up! Roberto Di Matteo takes Chelsea training ahead of their game with Barcelona              Di Mateo akitoa somo(training) wachezaji wake wa Chelsea jana mazoezini 

 Leader of the pack: Chelsea captain John Terry (centre) will be hoping to help Chelsea to a famous win   wachezaji wa Chelsea mazoezini jana tayari kuikabili Barca leo usiku

Main man? Didier Drogba and Fernando Torres will compete for the lone striking role            mazoezi makali......

All smiles: Lionel Messi shares a joke with Adriano at Stamford Bridge on Tuesday night
                                              Mnafurahia kichapo mtakachotoa auuu?????????

KUNA tatizo kwenye safu ya ulinzi ya Chelsea huku David Luiz akitarajiwa kukosekana kwenye mechi ya leo dhidi ya Barcelona baada ya kutolewa Uwanja wa Wembley dhidi ya Tottenham Jumapili. Mbali na kisiki hicho, Gary Cahill naye pia anasumbuliwa na maumivu ya mguu. John Terry ataendelea kucheza licha ya kwamba naye ni majeruhi na Branislav Ivanovic anaweza kuchukua nafasi ya Jose Bosingwa katika beki ya kulia, ambaye anatumikia adhabu aliyopewa katika Nusu Fainali ya Kombe la FA.
Training

Pamoja na hayo, Kocha Roberto Di Matteo lazima aamue kujenga imani juu ya wachezaji waliompa ushindi wa 5-1 dhidi ya Spurs. 
Pass masters: Barcelona are widely tipped to cruise past Chelsea and reach the finalwazee wa pass nao awa hapa mazoezini(Barca) Is that the way to Munich? Cesc Fabregas and Lionel Messi are plotting a route past Chelsea and into the Champions League final
Dider Drogba na Frank Lampard wote walifunga Jumapili, hivyo wana nafasi kubwa ya kuanza pamoja leo, ingawa Fernando Torres, ambaye alianza katika mechi zote dhidi ya Benfica, atakuwa na matumaini ya kuanza kwenye 11 wa kwanza.
Chelsea v Napoli

Barcelona haina majeruhi wapya na zaidi inafurahia kupona na kurejea kazini kwa wachezaji wake Dani Alves, Gerard Pique, Seydou Keita na Ibrahim Afellay. Lakini hatari moja tu kwao ni kwamba Javier Mascherano na Carles Puyol wana kadi moja moja za njano wote.

JE WAJUA?

Chelsea ilikutana mara ya mwisho na Barcelona Mei mwaka 2009, kwenye michuano kama hii na hatua kama hii. Baada ya sare ya bila kufungana kwenye mechi ya kwanza, Barca walifuzu kuingia fainali kwa bao la dakika ya mwisho la Andres Iniesta, ambalo lilikuwa la kusawazisha baada ya Michael Essien kutangulia kufunga. Barca ilifuzu kwa faida ya bao la ugenini.


•The Blues wana rekodi nzuri wakicheza nyumbani msimu huu katika Ligi ya Mabingwa. Vijana wa Di Matteo wamecheza mechi tano, wameshinda tano, wamefunga mabao 16 na wamefungwa mawili tu.


•Hii ni mara ya sita kwa timu ya London kucheza Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa ndani ya miaka tisa.


Lakini wameshinda mechi moja tu, walipoifunga kwa jumla ya mabao 4-3 mwaka 2008.


•Timu ya Stamford Bridge haijawahi kutwaa Kombe lolote la Ulaya, zaidi ya kushika nafasi ya pili mwaka 2008.


•Barcelona ilipokwenda mara ya mwisho London, Mei mwaka jana kwenye Uwanja wa Wembley, iliifungta Manchester United mabao 3-1 na kutwaa taji la nne la Ligi ya Mabingwa.


•Kama mabingwa hao watetezi watatwaa taji hilo msimu huu, itakuwa mara ya nne ndani ya miaka saba na itakuwa timu ya kwanza kutetea taji tangu AC Milan mwaka 1990.


•Huu ni msimu wan ne mfululizo, Barcelona inacheza Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa. Timu ya mwisho kuifunga Barca katika hatua hii, ilikuwa ni Inter Milan mwaka 2010.


•Lionel Messi amekutana na Chelsea mara sita katika Ligi ya Mabingwa, lakini hajawahi kutikisa nyavu za The Blues.


•Wakati timu hizo zilipokutana katika Robo Fainali mwaka 2000, Barcelona iliifunga Chelsea 5-1 katika mechi ya marudiano Uwanja wa Camp Nou.


Katika mechi hiyo, Roberto Di Matteo alicheza kwenye kikosi cha kwanza cha The Blues, wakati Pep Guardiola alichezea Barca- leo wote wanakaa kwenye mabenchi ya timu zao. Itakuwaje? Hili si game la kukosa.


VIKOSI VYA LEO: CHELSEA: Cech, Ivanovic, Terry, Cahill, Cole, Mikel, Lampard, Ramires, Mata, Kalou na Drogba.



BARCELONA: Valdes, Puyol, Mascherano, Pique, Alves, Xavi, Busquets, Iniesta, Sanchez, Messi na Pedro.

No comments:

Post a Comment