Hodgson mbioni kuutwaa umeneja wa timu ya taifa Egland
Roy Hodgson ndio ameibuka kuwa Mtu pekee anaeweza kuteuliwa kuwa Meneja wa Timu ya Taifa ya England baada ya Chama cha Soka England, FA, kuthibitisha kimepewa baraka na Klabu yake West Bromwich Albion ili kuongea nae rasmi kuhusu uteuzi huo.
Kumekuwa na dhana kubwa Meneja wa Tottenham Harry Redknapp ndie atakaepewa wadhifa huo ambao uko wazi tangu Februari baada ya kujiuzulu kwa Fabio Capello akipinga uamuzi wa FA kumuondoa John Terry kama Kepteni wa England kufuatia kuhusishwa na hatimae kushitakiwa kwa shutuma za kumtukana kibaguzi Mchezaji wa QPR Antoin Ferdinand ambae ni mdogo wake Mchezaji wa Manchester United Rio Ferdinand.
Roy Hodgson, Miaka 64, ameshawahi kuwa Meneja wa Timu za Taifa za Uswisi na Finland na pia Klabu kadhaa za Ulaya ikiwemo Inter Milan.
Akithibitisha habari hizi, Mwenyekiti wa FA, David Bernstein, ameishukuru WBA kwa ushirikiano wao wa kuwaruhusu kuongea na Hodgson ambae pia amewahi kuwa Meneja wa Liverpool kwa kipindi kifupi.
Enzi hizo Roy Hodgson (katikati) akiwa na bodi ya Bristol City mnamo mwaka 1982
Mkataba wa sasa wa Hodgson na WBA unamilizika Juni 30 Mwaka huu.
Kwa sasa England iko chini ya Meneja wa muda Stuart Pearce na Mechi zijazo inazozikabili England ni Mechi mbili za kirafiki na Norway huko Mjini Oslo hapo Mei 26 na nyingine na Belgium Uwanjani Wembley hapo Juni 2.
Kwenye EURO 2012, England ipo Kundi D na itacheza Mechi yake ya kwanza Mjini Donetsk, Ukraine hapo Juni 11 na Ufaransa.
KUNDI D
Ukraine
Sweden
France
England
MECHI ZAKE Kuchezwa Nchini Ukraine:
Juni 11: France v England [Mjini Donetsk Saa 1 Usiku]
Juni 11: Ukraine v Sweden [Kiev Saa 3 Dak 45 Usiku]
Juni 15: Sweden v England [Kiev Saa 1 Usiku]
Juni 15: Ukraine v France [Donetsk Saa 3 Dak 45 Usiku]
Juni 19: Sweden v France [Kiev Saa 3 Dak 45 Usiku]
Juni 19: England v Ukraine [Donetsk Saa 3 Dak 45 Usiku]
No comments:
Post a Comment