BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 3, 2012

KOCHA WA ITALIA AFUKUZWA KAZI NDANI YA MSIMU 1

Pasquale Marino
Genoa imemfukuza kocha wake Pasquale Marino na kumteua Alberto Malesani, ambaye anakuwa kocha wa 17 kufukuzwa katika Ligi Kuu Italia, Serie A yenye kushirikisha timu 20, tangu kuanza kwa msimu huu. Genoa ilitangaza hatua hiyo Jumatatu, timu hiyo ikiwa inashika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi hiyo, ikiwa imecheza mechi tisa bila kushinda, ya mwisho wakifungwa 5-4 na Inter Milan Jumapili. Hiyo inahusisha kufungwa mechi tano na sare nne.

Malesani alifukuzwa Desemba baada ya kipigo cha 6-1 kutoka kwa Napoli, lakini Genoa ilikuwa inalingana kwa pointi na timu inayoshika nafasi ya tisa kwenye ligi wakati huo.

No comments:

Post a Comment