BUKOBA SPORTS

Saturday, April 21, 2012

LIGI KUU ENGLAND: TIMU YA KWANZA KUSHUKA DARAJA WENDA IKAJULIKANA WIKIENDI HII



Huenda Timu ya kwanza kuporomoka Daraja Msimu huu ikajulikana Wikiendi hii huku Timu za kileleni zikipigana kuwania Ubingwa na nafasi muhimu.

Wolves, ambao ndio wako mkiani, wanaikaribisha Manchester City ambao wanasaka kupunguza pengo lao la Pointi 5 na vinara wa Ligi Mabingwa watetezi Manchester United ambao nao watakuwa kwao Old Trafford kucheza na Everton.


Ikiwa Wolves watafungwa au kutoka sare hatima yao kuporomoka Daraja itategemea matokeo ya Mechi za QPR v Tottenham na Bolton v Swansea.

Hata hivyo, Wolves wanahitaji miujiza ili wabaki Ligi Kuu.

Huku mbio za kusaka Ubingwa zikikolea kati ya Man United na Man City, zile za kusaka kuwemo 4 bora zitapamba moto kwa Chelsea, ambao wako furahani kwa kuitungua Barcelona juzi Jumatano kwenye Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, watakapotua Emirates kucheza na Arsenal.


DABI ZA LONDON

CHELSEA_V_ARSENALMechi ya kwanza kabisa kwa Wikiendi hii ni Dabi ya Jiji la London kwa Arsenal kuwa wenyeji wa Chelsea Uwanjani Emirates na hii ni Mechi muhimu kwa Timu zote zikiwania kuwemo 4 bora ili zicheze UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.

Kwa Chelsea ushindi ni lazima kwao kwa vile wapo nafasi ya 6 wakiwa Pointi mbili nyuma ya Timu iliyo nafasi ya 4 Tottenham ambayo imefungana kwa Pointi na Newcastle walio nafasi ya 5.

Arsenal wapo nafasi ya tatu na wapo Pointi 5 mbele ya Tottenham lakini walipoteza Mechi yao ya mwisho walipofungwa na Wigan bao 2-1 hivyo hawatakubali kufungwa kwa mara ya pili mfululizo na kuziruhusu Timu za nyuma yao kuwasogelea.

Kwenye mechi yao ya kwanza ya Ligi Msimu huu iliyochezwa Stamford Bridge hapo Oktoba 29, Arsenal waliifunga Chelsea bao 5-3 huku Robin van Persie akipiga hetitriki.

Tottenham, ambao Wikiendi iliyopita walifungwa bao 5-1 na Chelsea kwenye Nusu Fainali ya FA Cup, wapo ugenini kucheza na Queens Park Rangers katika Dabi nyingine ya Jiji la London.

Hii ni mechi ngumu kwa kila Timu kwani Tottenham wapo kwenye kinyang’anyiro cha 4 bora na QPR wao wako kwenye vita ya kujinasua kutoshushwa Daraja.


RATIBA:

Jumamosi Aprili 21
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Chelsea
[Saa 11 Jioni]
Aston Villa v Sunderland
Blackburn v Norwich
Bolton v Swansea
Fulham v Wigan
Newcastle v Stoke
[Saa 1 na Nusu Usiku]
QPR v Tottenham
Jumapili Aprili 22
[Saa 8 na Nusu Mchana]
Man United v Everton
[Saa 12 Jioni]
Liverpool v West Brom
Wolves v Man City


the dogfight

No comments:

Post a Comment