BUKOBA SPORTS

Monday, April 2, 2012

SIMBA NA YANGA ZASHINDA VPL


YANGA_V_SIMBA11 

MATOKEO:
Jumamosi Machi 31
Coastal Union 0 Yanga 1
Simba 2 African Lyon 0

Katika mechi za Ligi Kuu Vodacom zilizochezwa leo, wakongwe Yanga na Simba wote wameibuka na ushindi wakati Simba walipoichapa African Lyon 2-0 Jijini Dar es Salaam na Yanga kushinda 1-0 huko Tanga walikoifunga Coastal Union.
Mabao ya Simba yalifungwa na Salum Machaku na Haruna Moshi ‘Boban’ na ushindi huu, bila shaka, utawapa morali kubwa wakijiandaa kwa safari ya kwenda Algeria Siku chache zijazo kurudiana na ES Setif kwenye michuano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.
Simba waliifunga ES Setif bao 2-0 katika mechi ya kwanza.
Na katika mechi ya Coastal Union na Yanga huko Mkwakwani, Tanga bao pekee na la ushindi la Yanga lilifungwa na Hamisi Kiiza katika Dakika ya 85.

No comments:

Post a Comment