BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 24, 2012

UEFA CHAMPIONS LIGI LEO NOMA NI BARCA NA CHELSEA MARUDIANO

Centre of attention: Chelsea face Barcelona for a spot in the Champions League final on Tuesday night
Katika Miaka 9, hii ni mara ya 6 kwa Chelsea kucheza Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na wakiwa nafasi ya 6 kwenye Ligi Kuu England wana nafasi finyu kucheza Mashindano haya Msimu ujao kwani huenda wakakosa kufuzu kwenye 4 bora na njia pekee kucheza michuano hii Msimu ujao ni kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI.
 Leading the way: The Blues arrive in Barcelona with a slender 1-90 advantage over the Spanish giants
Alipoulizwa ikiwa watawamudu Barca ambao hawajafungwa katika Mechi 15 za Ulaya Uwanjani kwao Nou Camp, Meneja wa muda wa Chelsea, Roberto Di Matteo, alijibu: ‘Tuna uwezo kwenye Timu. Ukicheza ugenini unahitaji bahati lakini uwezo upo na Timu tunayo! Inabidi tufunge bao na kuzuia nafasi zote kwa Barca!’
 On the ball: Barca will be keen to bounce back from their 2-1 defeat at the hands of Real Madrid on Saturday
Nae Pep Guardiola, Meneja wa Barca, ambae alisakamwa kumchezesha Chipukizi Cristian Tello walipofungwa 2-1 na Real Madrid juzi Jumamosi, amesema: ‘Unaweza kuwashambulia Maveterani si Chipukizi. Chunguza si kuponda tu.’
Pia Meneja huyo wa Barca, ambayo haijapoteza Mechi 3 mfululizo kwa Miaka 9 sasa, ameonya juu ya tishio la Chelsea ambao Uwanjani Nou Camp watavaa Jezi nyeupe.
 Reach for the stars: Chelsea are looking for revenge after losing their 2009 semi-final against Barca

Guardiola ametamka: ‘Wana nguvu na wana silaha za kuweza kutuumiza, ni changamoto kubwa. Lakini sina wasiwasi tutafika Munich.’
 In charge: Guardiola oversees Barcelona's exciting brand of football

No comments:

Post a Comment