Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amekiri anaimisi na kuikumbuka sana Klabu yake ya zamani Manchester United na bado ana uhusiano mzuri na Sir Alex Ferguson.
Ronaldo alikaa Man United kwa Miaka 6 na kuhamia Real Madrid kwa dau la Pauni Milioni 80 Mwaka 2009.
Msimu huu, Ronaldo amezidi kung’ara huko Spain kwa kuvunja rekodi yake ya Msimu uliopita ya kufunga bao 40 katika La Ligi na Jumamosi iliyopita ndie aliefunga bao la ushindi Real ilipowachapa Barcelona bao 2-1 na kujichimbia kileleni mwa Ligi wakiwa Pointi 7 mbele ya Barca.
Ronaldo, akizungumzia Man United, amekiri: ‘Naongea na Sir Alex mara nyingine na nawakumbuka Wachezaji wenzangu. Kule ilikuwa kama Familia na nilikaa Miaka 6 na nina uhusiano mzuri sana na Ferguson na Wachezaji wote. Bado tunaongea na Rio Ferdinand, Nani, Anderson na Patrice Evra. Bado nawaona kama sehemu ya Familia.’
Alipoulizwa kitu kipi kinamkumbusha sana Sir Alex Ferguson, alicheka na kusema: ‘Ha! Nazimisi furaha zake za kila wakati! Daima yuko na furaha. Ha..ha!’
Pia alisema wakati wake bora akiwa na Man United ni pale walipotwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2008 kwa kuibwaga Chelsea.
Wakati akiwa na Man United, Ronaldo alitwaa Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani ya Mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment