BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 25, 2012

UEFA CHAMPIONZ LIGI: NANI KUTOKA KATI YA REAL MADRID AU BAYERN LEO?

Hard done by? Real Madrid boss Jose Mourinho (left) claims he's had bad luck in Champions League semi-finals

NUSU FAINALI==Marudiano:
[Mechi kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku Bongo Taimu]
[Matokeo Mechi za Kwanza katika mabano]
Jumatano Aprili 25
Real Madrid v Bayern Munich [1-2]
Game for a laugh: Cristiano Ronaldo (left) shares a joke with his Madrid team-mates in training 
Ronaldo akipeana maneno ya uchokozi na wachezaji wenzie jana kwenye mazoezi
Jumatano hii, ndani ya Santiago Bernabeu, Real Madrid wataingia uwanjani wakiwa na kazi moja tu ya kuupindua ushindi wa Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali wa Bayern Munich wa bao 2-1 walioupata Wiki iliyopita Uwanjani Allianz Arena ili wao watinge Fainali yao ya kwanza tangu Mwaka 2002 walipoutwaa Ubingwa wa Ulaya Uwanjani Hampden Park, Glasgow, Scotland walipoifunga Bayer Leverkusen kwa bao 2-1 kwa bao za Magwiji Raul na Zinedine Zidane.
 Just warming up: Real's squad prepare for the big game at Valdebebas training ground in Madrid

Lakini kuifunga Bayern Munich si kazi nyepesi kwa Kocha wa Real, Jose Mourinho, ambae amekiri kuwa huwa hana bahati na Nusu Fainali za UEFA CHAMPIONZ LIGI na pia akidokeza upendeleo wa Marefa ndio kikwazo, pale alipokumbusha amepoteza Nusu Fainali 3 kati ya 5 alizocheza.

Lying in wait: Bayern Munich playmaker Frank Ribery arrives in Madrid on Tuesday
Bayern Munich playmaker Frank Ribery alipowasili jana 

Alisema: ‘Sina bahati na Nusu Fainali! Nilipoteza moja na Liverpool wakati mpira haukuvuka mstari wa goli-huwezi kuamini hilo! Mwaka 2007, nilifungwa kwa penati-hiyo ni bahati mbaya! Msimu uliopita, Barca walitutoa Nusu Fainali na kila Mtu anajua ni kwanini!

Kuhusu Mechi na Bayern, aliongeza: ‘Ingawa tumefungwa Mechi ya kwanza kwa goli la ofsaidi, safari hii nategemea tutashinda tu!’

Mourinho amewahi kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI mara mbili, Mwaka 2004 akiwa na FC Porto na Mwaka 2010 akiwa na Inter Milan.
 Making a point: German duo Sami Khedira (second right) talks to Mesut Ozil (second left) in training

Lakini hatari kubwa inayomkabili Mourinho kutwaa Taji hili Msimu huu ni uwezekano wa kuwakosa baadhi ya Mastaa wake ikiwa watafika Fainali kwa vile Wachezaji kama Gonzalo Higuain, Xabi Alonso, Sergio Ramos na Fabio Coentrao, wamebakisha Kadi ya Njano moja tu ili wafungiwe kucheza Fainali ikiwa watafuzu.

Hata hivyo, Mechi hii ni ngumu mno kwa Real hasa kwa vile Bayern Munich, mbali ya kuongoza bao 2-1, pia wana motisha ya ziada kwa vile wakitinga Fainali wao watacheza Fainali hiyo Uwanja wao wa nyumbani Allianz Arena ambao ndio ulipangwa kufanyika Fainali hii tangu awali.

Katika Mechi za Wikiendi kwa Timu hizi walizocheza kwenye Ligi za nyumbani kwao, Bayern Munich waliifunga Werder Bremen bao 2-1 lakini walipata pigo pale Mabingwa watetezi Borussia Dortmund kuwachapa Borussia Monchengladbach bao 2-0 na kutwaa tena Ubingwa.

Real Madrid, wakicheza ugenini Uwanjani Nou Camp kwenye El Clasico, waliwachapa Mahasimu wao Barcelona bao 2-1 na kujizatiti kileleni mwa La Liga wakiwa Pointi 7 mbele ya Barcelona huku Mechi zimebaki 4.

Kwenye Mechi ya kwanza kati ya Bayern na Real Wiki iliyopita, Real ndio walitangulia kufunga Dakika ya 17 kwa bao la Franck Ribery na Real kusawazisha Kipindi cha Pili kupitia Kiungo wa Ujerumani Mezut Ozil katika Dakika ya 53.

Lakini katika Dakika za majeruhi, Mario Gomez aliipa ushindi Bayern kwa kupachika bao.

Watching brief: Mourinho looks on during training on the eve of the Champions League semi-final
Mourinhoakiwaangalia vijana wake kwenye mazoezi hiyo jana tayari kuwavaa Bayern

Mara ya mwisho Bayern Munich kucheza Santiago Bernabeu ilikuwa Mwaka 2010 kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIG walipofungwa na Inter Milan iliyokuwa chini ya Jose Mourinho.

No comments:

Post a Comment