Bondia Japhert Kaseba (kulia) akisaini mkataba wa kucheza pambano la ngumi na Francis Cheka siku ya sabasaba, (kushoto) ni Khalifa Kiumbemoto. Picha na Super D
BINGWA wa mchezo wa Kick Boxer, Japhet Kaseba, jana amesaini mkataba wa kucheza ngumi na
Bingwa wa dunia wa ndondi mkanda unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro katika uzani wa KG 75 utakaofanyika siku ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Bingwa wa dunia wa ndondi mkanda unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro katika uzani wa KG 75 utakaofanyika siku ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Kaseba amesema anashukuru kupata mpambano huo na atahakikisha anaonyesha uwezo wake katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mapambano.
''Najua mabondia wa hapa Bongo wananikwepa sana kwa kuwa nimeshakuwa bingwa wa ngumi za mateke lakini hawajui mimi ni bingwa katika mapigano yote'' alisema Kaseba.
Nitahakikisha najiandaa na mazoezi ya kutosha na kuweka kambi ya muda mrefu ili kukata ngebe za cheka kwani kwangu ni mtoto mdogo sana katika masumbwi, kwani mimi naamini Bingwa wa kweli ni Rashidi Matumla ambaye ninamuheshimu mpaka sasa, cheka kanikimbia muda mrefu tu tangu tupambane October 3, 2009 ambapo alipewa ubingwa kwa kusingizia mashabiki wangu walikuja kumtupa nje ya uwanja, tangua apo kazi yake yeye imekuwa ni kurudiana na Mada Maugo kila siku lakini kwa sasa kakanyaga miwaya zamu yake imefika,alisema Kaseba.
BUKOBASPORTS ITAKULETEA HABARI ZAIDI ZA MPAMBANO HUO NA SHOW ZINGINE
No comments:
Post a Comment