BUKOBA SPORTS

Thursday, April 5, 2012

USHAHIDI WA PICHA: REFA ALIKOSEA KUIPA PENATI BARCELONA DHIDI YA AC MILAN


FRAME 1: NESTA FOULING OUT OF PLAY

Katika hii fremu ya kwanza, Nesta anaonekana wazi kumshika na kumvuta Busquets huku kiungo wa Barca akijaribu kukimbilia mbele ya goli.

Kwenye sehemu ya kona, Xavi ndio kwanza alikuwa anajitaarisha kupiga kona. Kwa kuwa mpira ulikuwa haupo mchezoni, kosa la Nesta kumvuta jezi Busquets haliwezi kutolewa adhabu kwa kutoa penati.

Sheria za FIFA za 2011/12 zinasema: "Penati itatolewa ikiwa kosa limefanywa na mchezaji katika eneo la penati la timu yake, lakini lazima mpira uwe unaendelea yaani kosa liwe limefanyika mchezo ukiwa active.

Kwa maana hiyo, ikiwa mpira ulikuwa bado haujapigwa na Xavi basi hakukuwa na kosa ambalo lingemfanya refa atoe penati.

 

FRAME 2: NESTA & PUYOL FOULING OUT OF PLAY

Hii fremu ya pili, Xavi ndio anakaribia kupiga kona na bado hajagusa mpira. Nesta bado anaendelea kumvuta Busquets, lakini Carles Puyol nae anaingilia na anakaa kwenye njia ya Nesta na pia akaanza kumchezea ndivyo sivyo.

Na mpira ukiendelea kuwa nje ya mchezo, refa bado anakuwa hana mamlaka ya kisheria kutoa penati kutokanana sheria za FIFA. Mpaka kufikia pointi hii, kitu ambacho refa Kuipers inabidi na alitakiwa kupuliza filimbi yake, kusimamisha mchezo na kuuanzisha upya - baada ya kuongea na Nesta, Busquets na Puyol.


Huu ndio utaratibu refa anatakiwa kuufuata kutokana na maelekezo ya kanuni na sheria, linapotokea jambo kama lile ndani ya bo la penati. Kuipers ilibidi amuonye Nesta - na wachezaji wale wawili wa Barca - na hata angeweza kutoa kitabu chake. Na baada hapo angepuliza filimbi yake na kuanzisha upya mchezo.


Katika interview yake baada ya mchezo, Clerence Seedorf alielezea namna alivyo muuliza Kuipers kwanini alitoa penati. Lakini refa huyo alimjibu Nesta kwamba tayari alishamuonya Nesta kuhusu kuvutana kwenye box. Lakini swali linakuja kwanini alivyomuonya Nesta na mchezaji huyo akaendelea kumvuta Busquets, kwanini hakusimamisha mchezo na kumpa kadi Nesta? Nesta alikua kamshikilia Busquets kwa sekunde kadhaa kabla ya Xavi hajapiga mpira wa kona.




FRAME 3: PUYOL & NESTA FOULING IN PLAY

Wakati Xavi anapiga mpira wa kona, Nesta alijitahidi kwa kila hali kujaribu kumzuia Busquets asimtoroke, lakini akawa ameachwa kidogo. Puyol akawa amemshika Nesta kwa mikono yote miwili akijaribu kumzuia muitaliano huyo asiende mbele kumzuia Busquets.

Na sasa kwa kuwa mpira tayari ulikuwa upo mchezoni, kosa lolote ambalo lingetokea lingemaanisha penati kwa Barcelona au free kick kwa Milan.


Kibaya zaidi - mpaka hatua hii wote wawili Nesta na Puyol walikuwa wakitenda faulo. Kwa maana hiyo Milan wanaweza wakatoa hoja ya kwamba Nesta alikuwa akimvuta Busquets kabla ya mpira haujapigwa.






FRAME 4: PENALTY OR NO PENALTY?

Katika frame ya mwisho, kutokana na purukushani kabla ya mpra kupigwa kati ya Puyol, Nesta na Busquets - ilipelekea kiungo wa Barca kwenda chini. Nesta nae anaweza kusimama baada kusukumwa nje ya balance na Puyol.

Mpaka sasa, Refa tayari anakuwa ameshaweka filimbi yake mdomoni ili kutoa penati na kumpa kadi Nesta. Messi anachukua mpira na kufunga penati ile na kuwapa Barca uongozi wa 2-1.

Kukamilisha huu mjadala kuhusu hili tukio kupitia hizi picha - penati ile haikuwa halali kisheria - kwa sababu zifuatazo: Kwanza na muhimu kabisa, penati haiwezi kutolewa ikiwa mpira ukiwa umesimama yaani hauchezwi. Pili Refarii Kuipers alitakiwa kusimamisha mchezo na kuwaonya wachezaji au kutoa kadi kwa Nesta kwa kuchelewesha muda. Refa alikuwa na nafasi ya kufanya hivi kwa kuwa Nesta alikuwa kamganda Busquets kwa takribani sekunde nne kabla ya kona kupigwa. Tatu, na mpira baada ya kupigwa - penati sasa inaweza kutolewa lakini Puyol alikuwa akimfanyia madhambi Nesta kama ilivyokuwa sekunde chache kabla ya mpira kupigwa wakati Nesta alipokuwa akimtendea ndivyo sivyo Busquets.

No comments:

Post a Comment