BUKOBA SPORTS

Thursday, April 5, 2012

Di MATHEO: "CHELSEA BADO JOGOO"



Kaimu kocha wa Chelsea,Roberto Di Matteo anaamini klabu hiyo bado ina sifa ya kuwa klabu muhimu katika nyanja ya kimataifa licha ya kutowahi kamwe kunyakua kombe la ligi ya mabingwa wa Ulaya.
 Image text here
                            Hapa wakipeana neno na John Terry jana usiku
Ametoa kauli yake hiyo wakati Chelsea inajitayarisha na mkondo wa pili wa mechi ya robo fainali na Benfica ya Ureno. Chelsea ilishinda mkondo wa kwanza kwa bao moja kwa bila.
Wakiepuka kushindwa na Benfica siku ya Jumatano,watafaulu kuingia nusu fainali kwa mara ya sita katika misimu tisa ambapo watapambana na Barcelona.
"Mkiangalia muongo uliopita wa klabu hii,utaona imekuwa muhimu kitaifa na kimataifa.," alisema.
Kiungo Ramires nae pia alitamka kuwa klabu hiyo inaheshimiwa sana nchini kwao Brazil kama namna vilabu vya Barcelona au Real Madrid vinavyoheshimiwa.

No comments:

Post a Comment