Chelsea ina mipango ya kutobomoa mabomba ya kutolea moshi ikiwa itajenga uwanja mpya katika kituo cha Battersea
Chelsea imewasilisha ombi la kutaka kukinunua kituo cha kuzalisha umeme cha Battersea mjini London, na klabu kina mipango ya kujenga uwanja mpya wa soka mahali hapo, utakaoweza kuwapokea mashabiki 60,000.
Chelsea imeelezea imekuwa vigumu kupanua uwanja wao wa Stamford Bridge, na kiuchumi, mpango huo haufai, na vile vile klabu kimekuwa na matatizo katika kuwashawishi wahusika kuidhinisha mipango yake ya upanuzi.
Klabu kimeongezea kwamba kuna wengine wanaotaka kukinunua kituo hicho.
Uwanja wa sasa wa Chelsea(Stamford Bridge)
"Lazima pia kusisitiza kwamba kwa kuwasilisha ombi la kukitaka kituo cha Battersea cha kuzalisha umeme, hayo hayamaanishi moja kwa moja uamuzi kamili wa kuuhama uwanja wa Stamford Bridge."
Klabu kimeelezea kwamba kitazingatia masharti ya kutobomoa ukumbi uliopo katika eneo hilo na pia chumba cha kuendesha mitambo ya umeme, kwa kuzingatia sheria zinazohusiana na kuhifadhi majumba ya kale.
Naye Roman Abramovich anakubaliana na uongozi wa kuwa na kiwanja kikubwa (bigger stadium)
Klabu pia kina mipango ya kujenga maduka, nyumba na afisi katika eneo hilo, na vile vile kuimarisha usafiri kupitia treni za chini kwa chini.
No comments:
Post a Comment