BUKOBA SPORTS

Saturday, May 5, 2012

FAINALI FA CUP: MUDA MFUPI UJAO NI CHELSEA V LIVERPOOL USIKU HUU, FAINALI YA 131 YA FA CUP.

  Up for the cup: Chelsea and Liverpool clash at Wembley in the FA Cup final

DI MATTEO ANA REKODI 2 ZA FA CUP AMBAZO HAZIWEZI KUVUNJWA TENA!

TAREHE: 5 Mei 2012 UWANJA: WEMBLEY SAA: 1 na Robo Usiku [Bongo Taimu]

REFA: Phil Dowd


TATHMINI:
Meneja wa muda wa Chelsea, Roberto di Matteo, kesho ataiongoza Timu yake Uwanjani Wembley kucheza Fainali ya 131 ya FA Cup dhidi ya Liverpool huku yeye binafsi akiwa anashikilia Rekodi mbili za Kombe hili ambazo haziwezi kamwe kuvunjwa tena.
 Long walk: Liverpool fans set off in the morning for the trip down the motorway to Wembley
Akiwa Mchezaji wa Chelsea alifunga bao baada ya Sekunde 43 tu walipocheza Fainali dhidi ya Middlesbrough Mwaka 1997 na kunyakua Kombe na hilo ndilo lilikuwa bao la kufungwa mapema mno katika Fainali iliyochezwa Uwanja wa zamani wa Wembley kabla haujavunjwa.
 Di Matteo's double: The Chelsea manager won the FA Cup with Chelsea in 1997 against Middlesbrough and 2000 against Aston Villa
Di Matteo's double: The Chelsea manager won the FA Cup with Chelsea in 1997 against Middlesbrough and 2000 against Aston Villa
Pia bao lake la ushindi kwenye Fainali ya FA Cup dhidi ya Aston Villa Mwaka 2000 lilikuwa ndio bao la mwisho kabisa kufungwa kwenye huo Uwanja wa zamani wa Wembley.
Akiongelea Fainali hiyo, Di Matteo amesema: ‘Ni muhimu twende mbele. Tunataka kutwaa FA Cup na UEFA CHAMPIONZ LIGI lakini ingawa tumefanya vizuri kutinga Fainali lakini bado hatujashinda!’
Di Matteo's double: The Chelsea manager won the FA Cup with Chelsea in 1997 against Middlesbrough and 2000 against Aston Villa
15.55: Chelsea boss Roberto Di Matteo has fond memories of FA Cup finals for Chelsea at Wembley
Meneja wa Liverpool, Kenny Dalglish, anachukulia kutwaa Kombe hili kwa umuhimu mkubwa hasa baada ya kutofanya vizuri kwenye Ligi Kuu England.
Liverpool tayari wana Taji moja Msimu huu baada ya kutwaa Carling Cup Mwezi Februari walipoifunga Cardiff City kwa mikwaju ya penati.
HALI ZA WACHEZAJI:
Didier Drogba na Mchezaji wa zamani wa Liverpool Fernando Torres inaelekea wanapigania nafasi moja ya Straika atakaechezeshwa kwenye Kikosi cha Chelsea.
Majeruhi wa Chelsea ni Mabeki Gary Cahill na David Luiz.
Mbali ya majeruhi wa muda mrefu Viungo Lucas Leiva na Charlie Adam, Liverpool hawana tatizo jingine na watawachezesha Straika Luis Suarez na Nahodha Steven Gerrard ambao walipumzishwa kwenye Mechi ya majuzi Jumanne walipofungwa na Fulham.

USO KWA USO:
• Kati ya Mechi za Ligi na Makombe 162 ambazo Chelsea na Liverpool wamekutana katika Miaka 105, Liverpool wameshinda Mechi 73, sare 33 na wamefungwa 56.
• Msimu huu Jumamosi itakuwa mara ya 3 kukutana na katika mara mbili walizocheza Liverpool alishinda Mechi zote, 2-1 kwenye Ligi na 2-0 kwenye Raundi ya 5 ya Carling Cup mechi zote zikichezwa Uwanjani Stamford Bridge.

RIPOTI YA AWALI
FAINALI FA CUP: Chelsea v Liverpool
TAREHE: 5 Mei 2012 UWANJA: WEMBLEY SAA: 1 na Robo Usiku [Bongo Taimu]
REFA: Phil Dowd

Hii itakuwa ni Fainali ya 131 ya FA Cup, ambayo ndio Mashindano ya zamani kabisa ya Kombe kushindaniwa ndani ya Nchi, na safari hii Mechi kati ya Chelsea na Liverpool itachezwa kwa mara ya kwanza chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia aina ya Budweiser.
Tarehe ya pambano hili itaingiliana na Mechi za Ligi Kuu England na ili kuepuka hilo Fainali hii itachezwa baada ya Mechi za Ligi Siku hiyo kumalizika na litaanza Saa 1 na Robo Usiku, Saa za Bongo.
Pia, Fainali hii imesogezwa, na ndio maana ikaingiliani na Mechi za Ligi ili kutoa pengo la Wiki 4 baada ya kumalizika Ligi na kabla kuanza yale Mashindano makubwa ya UEFA EURO 2012.

KLABU ZINAZOONGOZA KUTWAA FA CUP MARA NYINGI:
-Manchester United Mara 11  (1909, 1948, 1963, 1977, 1983, 1985, 1990, 1994, 1996, 1999, 2004)
-Arsenal 10
-Tottenham 8
-Liverpool 7
-Aston Villa 7

TATHMINI:
Hii itakuwa mara ya 14 kwa Liverpool kutinga Fainali ya FA Cup na wametwaa Kombe hili mara 7, katika Miaka ya 1965, 1974, 1986, 1989, 1992, 2001 na 2006 na wamefungwa mara 6 kwenye Fainali katika Miaka ya 1914, 1950, 1971, 1977, 1988 na 1996.
Kwa Chelsea ni mara ya 11 kutinga Fainali na wamenyakua Kombe mara 6 Miaka ya 1970, 1997, 2000, 2007, 2009 na 2010 na kufungwa mara 4 katika Miaka ya 1915, 1967, 1994 na 2002.
Liverpool na Chelsea wameshakutana mara 9 kwenye FA Cup, zikiwemo Nusu Fainali mbili, lakini hawajawahi kukutana Fainali.
Katika mara hizo 9 walizokutana, Chelsea wameshinda mara 5 na Liverpool mara 4 lakini kwenye hizo Nusu Fainali mbili walizovaana, Liverpool alishinda zote.
Kombe pekee ambalo Chelsea na Liverpool wamekutana kwenye Fainali ni lile la Ligi Cup [siku hizi Carling Cup] walipocheza Mwaka 2005 Uwanja wa Millenium Mjini Cardiff na Chelsea kushinda bao 3-2.
Siku hiyo ya Fainali ya FA Cup, Mei 2, 2012, Liverpool na Chelsea zilikuwa zicheze Mechi kati yao ya Ligi Kuu England Uwanjani Anfield lakini sasa Mechi hii itachezwa Jumanne Mei 8.
Kila Klabu imepewa mgawo wa Tiketi 25,074 za kununuliwa na Mashabiki wao kwa ajili ya Fainali hiyo na Tiketi nyingine kusambazwa katika sehemu mbalimbali ya jamii za Soka huku Tiketi 17,000 zimetengwa kwa Wanachama wa Club Wembley ambao ni wale wenye Tiketi za Msimu kwa ajili ya Mechi zichezazwo Uwanja wa Wembley.
NJIA ILIYOWAFIKISHA WEMBLEY:
[FAHAMU: Klabu za Ligi Kuu England huanza FA Cup kwenye Raundi ya 3]
CHELSEA
-Raundi ya 3: Chelsea 4 Portsmouth 0
-Raundi ya 4: QPR 0 Chelsea 1
-Raundi ya 5: Chelsea 1 Birmingham 1
-Marudiano: Birmingham 0 Chelsea 2
-Raundi ya 6: Chelsea 5 Leicester City 2
-Nusu Fainali: Chelsea 5 Tottenham 1
LIVERPOOL
-Raundi ya 3: Liverpool 5 Oldham Athletic 1
-Raundi ya 4: Liverpool 2 Man United 1
-Raundi ya 5: Liverpool 6 Brighton & Hove Albion 1
-Raundi ya 6: Liverpool 2 Stoke City 1
-Nusu Fainali: Liverpool 2 Everton 1

No comments:

Post a Comment