BUKOBA SPORTS

Sunday, May 6, 2012

NGORONRO HEROES YASONGA MBELE, YAWATUPA NJE SUDAN

Ulimwengu, mfungaji wa bao la Ngorongoro
TIMU ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imefanikiwa kusonga mbele katika kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika, baada ya kutioa Sudan kwa jumla ya mabao 4-3.






Katika mchezo wake wa jana usiku, Ngorongoro imekubali kipigo cha mabao 2-1 ugenini, kwenye Uwanja wa Khartoum, baada ya awali kushinda 3-1 Uwanja nyumbani wa Taifa, Dar es Salaam wiki mbili zilizopita na sasa itachuana na Nigeria Raundi ya Pili, mechi ya kwanza ikicheza Julai 28, mwaka huu Dar es Salaam.

Sudan walipata mabao yao kupitia kwa Mohammed Abdelrahman, katika dakika ya 10 na Ahmad Nasr kwa penalti dakika ya 65, wakati bao la Ngorongoro lilifungwa na mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwengu kabla ya mapumziko.

Ngorongoro Heroes wanatarajia kurejea nchini leo Jumapili majira ya Saa 3 asubuhi.

Mshindi kati ya Ngorongoro na Nigeria atamenyana na mshindi kati ya Afrika Kusini na Kongo Brazzaville, mechi ya kwanza ikichezwa kati ya Septemba 21 na 23 mwaka huu ugenini na marudiano Oktoba 6.
                                WWW.BUKOBASPORTS.BLOGSPOT.COM

No comments:

Post a Comment