Viongozi wanaofuatana na timu hiyo ni Ismail Aden Rage (MB), Swedy Fikirini Mkwabi, Milovan Cirkovic, Amatre Richard, James Stephan Kisaka, Dk. Cosmas Kapinga, Nicholaus Menrad Nyagawa na Ezekiel Kamwaga. Mkuu wa msafara huo atakuwa ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Hussein Mwamba.
Wachezaji wawili; Nassor Said Masoud (Chollo) na Juma Said Nyoso hawatakwenda Sudan kwa vile wanatumikia adhabu zao za kukosa mechi kutokana na kuwa na kadi. Mechi ya Shandi na Simba itapigwa Jumapili ijayo katika Uwanja wa Shandi wenye uwezo wa kuchukua washabiki 10,000. Mji wa Shandi uko Kaskazini Magharibi mwa Sudan na uko umbali wa kilomita 150 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
No comments:
Post a Comment