BUKOBA SPORTS

Wednesday, May 2, 2012

LA LIGA: CIBELES KUWAKA MOTO LEO?

 
 CEBELES NDIKO MASHARIKI WA REAL MADRID HUJUMUIKA KUSHEREKEA TAJI!
Mara ya mwisho Mashabiki wa Real Madrid kuvamia sehemu yao maalum kusherehekea Taji ilikuwa ni Mwaka jana walipotwaa Copa del Rey baada ya kuwabomoa Mahasimu wao Barcelona lakini Mashabiki hao hawajatua Chemchem ya Cibeles, iliyo katikati ya Jiji la Madrid, kusherehekea Ubingwa wa Spain tangu Mwaka 2008 kwani Taji limekuwa likienda Jijini Barcelona tangu wakati huo.
Lakini leo Usiku, Timu yao Real Madrid, ipo ugenini Estadio San Mames kucheza na Athletic de Bilbao na ushindi kwenye Mechi hii utawapa Ubigwa na kuwafanya Mashabiki wao waivamie Cibeles kwa shangwe kubwa.
Hata hivyo, Real wanaweza kuwa Mabingwa leo kabla ya kucheza na Bilbao kwa vile Barcelona wanacheza na Malaga mapema, Saa 3 Usiku na Mechi ya Real inaanza Saa 5 Usiku, na ikiwa Barca watafungwa Ubingwa moja kwa moja unaenda Real kwa vile wapo mbele kwa Pointi 7 ya Barca ambao watakuwa wamebakisha Mechi mbili tu.
Pichani ni Nahodha wa Real Iker Casillas akivalisha Sanamu ya Cibeles Skafu ya Real Madrid walipotwaa Copa del Rey Mwaka 2011. 

                   MECHI ZILIZOBAKI:
     REAL MADRID
-Athletic Bilbao [Ugenini]
-Granada [Ugenini]
-Real Mallorca [Nyumbani]

     BARCELONA
-Malaga [Nyumbani]
-Espanyol [Nyumbani]
-Real Betis [Ugenini]

RATIBA / MATOKEO-LA LIGA:
Jumanne Mei 1
Getafe 1 Real Racing Santander 1
Granada 2 Espanyol 1
Sporting Gijon 2 Villareal 3
Jumatano Mei 2
Atletico Madrid v Real Sociedad
Barcelona v Malaga [Saa 3 Usiku]
Real Mallorca v Rayo Vallecano
Sevilla v Real Betis
Real Zaragoza v Levante
Athletic Bilbao v Real Madrid [Saa 5 Usiku]
Valencia v Osasuna

No comments:

Post a Comment