BUKOBA SPORTS

Wednesday, May 2, 2012

LIGI KUU ENGLAND: CHELSEA V NEWCASTLE, BOLTON VS SPURS SAA 3:45

Wakiwa wamo kwenye Fainali za FA Cup na UEFA CHAMPIONZ LIGI ambazo zote zinachezwa Mwezi huu Mei.
 
Chelsea sasa wanaingia kwenye kipindi muhimu kwao na leo wapo kwao Stamford Bridge kucheza na Newcastle Timu ambayo iko juu yao tu katika nafasi ya 5 ikiwa Pointi moja mbele yao.
 
Chelsea itawakosa Masentahafu David Luis na Gary Cahill kwa vile ni majeruhi lakini watakuwa nae Branislav Ivanovic ambae ndio anatoka kifungoni.
Newcastle wao hawana majeruhi na wana Kikosi kamili.




BOLTON V TOTTENHAM 
FABRICE MUAMBA KUTINGA UWANJANI KUSHUHUDIA MECHI YA TIMU YAKE!!! 
 
Leo Uwanjani Reebok, Mashabiki wanategemewa kumkaribisha Kiungo wa Bolton Fabrice Muamba ambae anategemewa kukaa Jukwaani baada ya kupona alipodondoka ghafla Uwanjani White Hart Lane na kupoteza fahamu wakati Tottenham inacheza na Bolton kwenye Kombe la FA.
 
 Heartache: The players were left stunned after Muamba (above, centre) collapsed at White Hart Lane (below)

No comments:

Post a Comment