BUKOBA SPORTS

Monday, May 7, 2012

LIGI KUU ENGLAND: MAN CITY YAZIDI KUNYEMELEA UBINGWA, YAIFUNGA NEWCASTLE 2-0

We're almost there: Manchester City boss Roberto Mancini celebrates
Bosi wa  Manchester City (Roberto Mancin) akishagilia ambavyo na tofauti na siku nyingine!!!
Sky Blue heaven: Yaya Toure celebrates his second goal
Yaya Toure akishangilia goli lake la pili
Manchester City imesogea karibu kabisa ya mfundo wa kumalizia Ligi Kuu ya England na kutangazwa mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 44, baada ya Yaya Toure kufunga mabao mawili na kuipatia ushindi wa mabao 2-0 timu yake dhidi ya Newcastle United.Crucial strike: Toure tucks home the opener
Kiungo huyo anayechezea pia timu ya taifa ya The Ivory Coast alifanikiwa kumfunga mlinda mlango Tim Krull kwa mkwaju maridadi wa kimo cha beberu zikiwa zimesalia dakika 20 kabla mpira kumalizika.City slickers: Toure is mobbed by his team-mates after his second goal at St James' Park
Baadae kidogo Yaya Toure akaongeza bao la pili kwa mkwaju wa karibu huku muda nao ukiwa umewatupa mkono Newcastle.
Manchester City sasa wanafahamu fika iwapo watafanikiwa kupata ushindi dhidi ya QPR katika mechi ya kumalizia msimu, basi watatangazwa moja kwa moja mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya kandanda ya England.
Ulikuwa ni mchezo murua hasa kwa Manchester City wakiongozwa na nahodha wao Vincent Kompany safu ya ulinzi, huku David Silva akitawala eneo la kiungo na umaliziaji uliofana wa Toure akishirikiana na kikosi kizima wakihakikisha hawafanyi makosa kulikosa kombe msimu huu.
Ulikuwa uwanja huo huo wa Newcastle tarehe 11 mwezi wa Mei mwaka 1968 ambapo Manchester City walinyakua ubingwa wa ligi kwa mara ya mwisho. Takriban miaka 44 baadae inaonekana historia ipo njiani kujirudia huku klabu hiyo ikisogea mbele ya Manchester United ambao waliokuwa wanaongoza ligi hiyo kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment