BUKOBA SPORTS

Tuesday, May 8, 2012

LIGI KUU ENGLAND: WIGAN WAENDELEZA KICHAPO WAIFUNGA BLACKBURN WAISHUSHA DARAJA, TIMU MOJA KUSHUKA DARAJA MEI 13

Blackburn Rovers fans launched a protest via this feathered friendkuku awatemesha ushindi Blackburn
We're up! Antolin Alcaraz (second left) leads the celebrations as Wigan won Premier League survival
 Antolin Alcaraz (wa pili kushoto) akishangilia Wigan kupanda daraja (Premier League survival)
Bao la Dakika ya 87 la Antolin Alcaraz kwenye Mechi ya Ligi kuu England iliyochezwa jana Ewood Park limewapa Wigan ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Blackburn Rovers na kuhakikisha usalama wao kubaki Ligi Kuu England na pia kuwaporomosha Daraja Blackburn Rovers ambao wanaungana na Wolves kucheza Ligi ya Npower Championship Msimu ujao.

Hadi sasa bado kujulikana Timu ya 3 itakayoungana na Blackburn na Wolves kushuka Daraja lakini itakuwa ni kati ya Bolton, QPR au hata Aston Villa ingawa hawa wanalindwa na ubora wa tofauti ya magoli.
 Match-winner: Antolin Alcaraz (fourth left) heads in the decisive goal at Ewood Park

Kwa muda mrefu Mashabiki wa Blackburn wameonekana  wakilalamika kumpinga Meneja Steve Kean pamoja na Wamiliki wa Klabu hiyo, Kampuni ya kuuza Kuku ya Kihindi Venky’s, na jana mmoja wa Mashabiki hao alimtoa Kuku alievalishwa Jezi ya Blackburn na Kuku huyo akatinga Uwanjani kwenye Dakika ya 8 na kusababisha pambano lisimame hadi pale Kipa wa Wigan, Al Habsi, alipomnyakua Kuku huyo na kuwapa Walinzi.
 Pitch invader: A chicken was released in protest against Blackburn owners, Venky's
Kabla ya Mechi za mwisho za Ligi Kuu England kwa Msimu huu kuchezwa Jumapili ijayo Mei 13, Jana  timu ya Wigan ilifanikiwa Usiku kuifunga Blackburn goli 1-0 kwa kile  kiporo cha  Mechi yao, Blackburn Rovers walikuwa kwao kupigana na Wigan Athletic kwenye Mechi ambayo ilikuwa ngumu sana na  muhimu kwa vile kila Timu ilikuwa inawinda ushindi ili kujinusuru balaa la kushushwa Daraja. mfungaji wa bao hilo akiwa ni Antolin Alcaraz goli la kichwa la dk ya 87.
Down and out: Steve Kean sees Blackburn relegated
Steve Kean baada ya timu yake kufungwa alionekana kuchoka na huku kelele za mashabiki zikizidi
Making their point: Blackburn fans made their feelings about Steve Kean known during the game
Katika mchezo huo mashabiki wa Timu ya Blackburn walinyoosha mabango juu yakimtaka kiongozi wa timu hiyo kujiuzuru na mengine yakiandiwa (Steve Kean nje!)
Kituko, mechi ikiendelea alionekana kuku wa Blackburn uwanjani na mechi kusimamishwa kwa muda mpaka alipokamatwa na kipa Ali Al Habsi kwa kushirikiana na Yakubu, kuku huyo kuchukuliwa na polisi nje wa uwanja.
VIKOSI
Blackburn: Robinson, Orr, Dann, Givet, Martin Olsson, Hoilett, Dunn, Lowe, Pedersen, Modeste, Yakubu
Akiba: Kean, Formica, Petrovic, Nzonzi, Rochina, Marcus Olsson, Goodwillie.
Wigan: Al Habsi, Alcaraz, Caldwell, Figueroa, Boyce, McArthur, McCarthy, Beausejour, Moses, Di Santo, Maloney
Akiba: Pollitt, Crusat, Ben Watson, Gomez, Sammon, Rodallega, Diame.
Refa: Mark Clattenburg

Game for a laugh: Yakubu and Ali Al Habsi watch on as the cockerel makes its way across the pitch
                     Yakubu na Ali Al Habsi wakiwa kwenye kamata kamata ya kuku uwanjani
To the rescue: Wigan goalkeeper Al Habsi catches the cockerel in the goal-net
                              Al Habsi akafanikiwa kumkamata kuku huyo kwenye neti za goli
Hanging their heads: Blackburn's Marcus Olsson and Yakubu walk from the pitch after being relegated
Dejection: Paul Robinson trudges off after Blackburn were relegated 
Adui wa Rovers iliyohitaji ushindi tu kwenye mechi ya jana ili kubaki Ligi Kuu alikuwa ni Antolin Alcaraz aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 87 Uwanja wa Ewood Park.




Barclays Premier League
PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Man City37275590276386
2Man Utd37275588335586
3Arsenal372071071472467
4Tottenham37199964412366
5Newcastle37198105548765
6Chelsea361710962412161
7Everton371411124739853
8Fulham371410134849-152
9Liverpool361310134338549
10West Brom37138164349-647
11Sunderland371112144545045
12Swansea371111154351-844
13Norwich371111155066-1644
14Stoke371111153451-1744
15Wigan371010173960-2140
16Aston Villa37717133751-1438
17QPR37107204163-2237
18Bolton37105224475-3135
19Blackburn3787224776-2931
20Wolverhampton37510223879-4125

No comments:

Post a Comment