Vincent Kompanyakishangilia baada ya kuipatia Man city Goli jana usiku
Kompany akitupia kwa kichwa ndani ya goli la watani wao City( Man City walishinda 1-0)
Huku Mechi zikiwa zimebaki mbili Ligi Kuu England kumalizika, Manchester City leo wameitungua Manchester United bao 1-0 na wanauchungilia Ubingwa wao wa kwanza tangu Mwaka 1968 ikiwa watazifunga Newcastle ugenini na QPR nyumbani na Man United kuteleza tena wakicheza na Swansea nyumbani na Sunderland ugenini.
Mpira wa kona katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza uliopigwa na David Silva uliunganishwa na nahodha Vincent Kompany na kumpita kipa David De Gea na kuandika ndio bao pekee lililodumu hadi mwisho.
Diego Maradona akimwangalia mkwe(son-in-law) Sergio Aguero akifanya vitu uwanjani jana
Ushindi huu wa bao la kichwa la Kompany katika Dakika ya 46 umewafanya Man City wafungane Pointi na Man United lakini wao wako kileleni kwa ubora wa tofauti ya magoli.
VIKOSI
Manchester City: Hart, Zabaleta, Lescott, Kompany, Clichy, Barry, Toure Yaya, Silva, Tevez, Nasri, Aguero.
Akiba: Pantilimon, Richards, Milner, Dzeko, Kolarov, De Jong, Balotelli.
Manchester United: De Gea, Jones, Ferdinand, Smalling, Evra, Nani, Carrick, Scholes, Park, Giggs, Rooney.
Akiba: Amos, Berbatov, Hernandez, Young, Welbeck, Rafael Da Silva, Valencia.
Refa: Andre Marriner
RATIBA:
Jumanne Mei 1
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Liverpool v Fulham
Stoke v Everton
Jumatano Mei 2
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Newcastle
[Saa 4 Usiku]
Bolton v Tottenham
MSIMAMO WA TIMU ZA JUU:-
1 Man City Mechi 36 Pointi 83 [Tofauti ya Magoli 61]
2 Man United Mechi 36 Pointi 83 [54]
3 Arsenal Mechi 36 Pointi 66 [24]
4 Tottenham Mechi 35 Pointi 62 [20]
MSHIKE MSHIKE NAO HAUKUKOSA WAZEE WA TIMU NAO WALIZOZANA KIAINA!
Sir Alex Ferguson na Roberto Mancini walizozana baada ya Nigel De Jong kumkata Danny Welbeck
Hapa inaonekana walitupiana maneno makali sasa sijui aliyeanza nani? ntakujuza baadaye ....
Nachojiuliza mechi ilipoisha walipeana mikono au vp?
No comments:
Post a Comment