BUKOBA SPORTS

Friday, May 4, 2012

MIAKA 20 LIGI KUU ENGLAND: GOLI BORA NI LA ROONEY ALIPOIFUNGA MAN CITY FEBRUARY 2011

Wayne Rooney of Manchester United
Bao la Tiki Taka(spectacular overhead kick) la Wayne Rooney alipofunga wakati Manchester United ilipoitwanga Manchester City 2-1 Februari 2011  ndilo limepigiwa kura na Mashabiki Dunia nzima kuwa ndilo Goli Bora katika Miaka 20 ya Ligi Kuu England kwa asilimia 26%

Goli lililoshika nafasi ya pili ni lile la Dennis Bergkamp la Mwaka 2002 alipobetua mpira juu na kugeuka na kuwadaa Mabeki wa Newcastle na kuifungia Arsenal bao kwa asilimia 19%.
 
Bao la 3 ni la Mchezaji mwingine wa Arsenal, Thiery Henry, alilofunga Mwaka 2000 dhidi ya Manchester United kwa asilimia 15%.
 
Katika kuadhimisha Miaka 10 ya Ligi Kuu, David Beckham, alipokuwa na Manchester United, alishinda Tuzo ya Goli Bora katika Miaka 10 ya Ligi Kuu England.
Akishukuru baada ya goli lake kuteuliwa Bora, Rooney alisema: ‘Tangu mdogo nimekuwa nikitazama Ligi Kuu na kuteuliwa Goli langu ni bora inanifanya nijisikie vizuri. Natoa shukrani zangu kwa Mashabiki walionipigia kura.’

No comments:

Post a Comment