BUKOBA SPORTS

Friday, May 4, 2012

MILOVAN: TUTAWAFUNGA YANGA NA KUCHUKUA UBINGWA!

KOCHA Mkuu wa Simba, Mserbia Milovan Cirkovic ametamba kikosi chake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayofikia tamati hivi karibuni.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Zanzibar ambapo timu yake imeweka kambi, Cirkovic alisema kutokana na hali ilivyo, kikosi chake kinampa moyo kwamba kinaweza kushindana katika michuano yoyote.
“Kikosi changu kiko vizuri na kina uwezo wa kushinda mechi yoyote inayokuja mbele yake hata ya marudiano dhidi ya Al Ahly Shandy itakayofanyika Sudan,” alisema.
Simba inakabiliwa na mechi ya marudiano ya raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya timu hiyo inayotarajiwa kufanyika Sudan katikati ya mwezi huu ambapo timu hiyo imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele baada ya kushinda mabao 3-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


"Nina imani na kikosi changu kutokana na hali iliyokuwa nayo...nina uhakika kitafanya vizuri dhidi ya Yanga na hata katika mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho," alisema Cirkovic.

No comments:

Post a Comment