BUKOBA SPORTS

Friday, May 4, 2012

KOCHA FIORENTINA AFUKUZWA, AFUNGIWA MIEZI MITATU NA SERIE A, KISA KUMPIGA MCHEZAJI.

KISA: Kumtwanga Mchezaji kwenye Mechi ya Serie A!!

Shock: Ljajic (right) heads back to the bench after being substituted - and then attackedMara baada ya kufukuzwa na Klabu yake Fiorentina, Kocha Delio Rossi, amelikwaa rungu jingine baada ya Wasimamizi wa Serie A kuamua kumfungia Miezi mitatu kwa kosa la kumshambulia Mchezaji wake Raia wa Serbia Adem Ljajic kwenye Mechi ya Serie A jana Jumatano ambayo Fiorentina walitoka sare 2-2 na Novara.

Hurt: Ljajic (right) looked visibly upset as he sat on the bench after being hit by Rossi
 Ljajic (kulia) aliyepigwa na  Rossi akiwa benchi kwa mfadhaiko sana na kukwazika kwa kichapo hicho.
Serie A imetangaza kuwa imemwadhibu Delio, Miaka 51, baada ya kuchunguza ushahidi wa TV ambao ulionyesha kuwa Ljajic akiitolewa Uwanjani na kubadilishwa katika Dakika ya 32 na aliporudi na kukaa kwenye Benchi akaanza kushangilia huku akimdhihaki Kocha Delio na ndipo Rossi akaruka na kuanza kumpiga hadi alipovutwa na wengine waliokuwa hapo Benchi.
Mara baada ya tukio hilo mmiliki wa Fiorentina aliamua kumfukuza kazi Kocha huyo.

No comments:

Post a Comment