BUKOBA SPORTS

Friday, May 4, 2012

LIGI KUU ENGLAND: NEWCASTLE NA TOTTENHAM ZASHIKANA MASHATI KUGOMBEA NAFASI YA KUCHEZA CHAMPIONS

MAJEMBE YA NEWCASTLE YENYE USONGO
Zile mbio za kumaliza 4 bora ili kucheza Ulaya Msimu ujao zimeingia patamu baada ya juzi wagombea wake Tottenham na Newcastle wote kushinda ugenini.
MSIMAMO WA NEWCASTLE NA SPURS ULIVYO KWA SASA.
[Kila Timu imecheza Mechi 36]

4 Tottenham 65 [Tofauti ya Magoli 23]
-------------------------------------
5 Newcastle 65 [tofauti ya Magoli 9]

Bao mbili za Papiss Demba Cissé Uwanjani Stamford Bridge ziliwafanya Newcastle waifunge Chelsea bao 2-0 na kuwafanya Newcastle wakamate nafasi ya 5 wakifungana kwa Pointi na Tottenham ambao wako juu kwa ubora wa magoli tu.
Newcastle na Tottenham, zote zina Pointi 65, na zipo Pointi 1 tu nyuma ya Arsenal.
Kipigo hicho kimewafanya Chelsea wabaki nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 61.
Nao Tottenham, wakicheza Uwanja wa Reebok, waliichapa Bolton bao 4-1 kwa bao za Luka Modric, Rafael van der Vaart na mbili za Emmanuel Adebayor.

 
MAJEMBE YA TOTTENHAM

No comments:

Post a Comment