BUKOBA SPORTS

Friday, May 18, 2012

NANI KUCHUKUA MIKOBA YA DALGLISH LIVERPOOL KATI YA (ROBERTO MARTINEZ , BRENDAN RODGERS, FABIO CAPELLO AU PEP GUARDIOLA ) ???

Wigan imeiruhusu klabu ya Liverpool kushauriana na meneja Roberto Martinez, ikiwa atakubali kuiongoza klabu hiyo ya uwanja wa Anfield.

Tajiri wa Wigan, Dave Whelan amethibitisha habari hizo.
Kenny Dalglish, aliyekuwa meneja, alifutwa kazi siku ya Jumatano, na klabu ya Liverpool inamtafuta kocha wa nne katika kipindi cha miaka miwi.
 
"Nilitoa idhini kwa Liverpool kuzungumza na Roberto na watazungumza naye hivi punde", Whelan aliwaelezea waandishi wa habari wa michezo wa Sky.
Uongozi wa Liverpool umo katika kuwatafuta watu ambao huenda wakafaa kuchukua kazi hiyo, ikiwa ni pamoja na meneja wa Swansea, Brendan Rodgers.
 Wanted: Pep Guardiola is free after leaving Barcelona
Martinez alikuwa meneja wa Swansea mwezi Februari, mwaka 2007, na kuiwezesha timu kufika hadi daraja ya kwanza.
Whelan amesema anatumaini Martinez ataamua kusalia katika uwanja wa DW, lakini anafahamu umaarufu wa meneja huyo Mhispania. 
 On the shortlist: Former England boss Fabio Capello has also been approached by Liverpool
"Sijui Roberto ana hisia zipi kuihusu klabu ya Liverpool.
Nadhani atakuwa akielekea huko akiwa tayari kwa lolote.
Lakini ningelipenda Roberto kubaki".
 The last straw: Swansea boss Brendan Rodgers (right) oversaw Swansea's 1-0 victory over Liverpool in Kenny Dalglish's final match in charge

No comments:

Post a Comment