BUKOBA SPORTS

Thursday, May 10, 2012

PEKUPEKU MPAKA KUJA KUWA MWANASOKA TAJIRI DUNIANI: NJIA ALIZOPITIA YAYA TOURE KUFIKA HAPA ALIPO.

 Young at heart: Toure (centre) as a boy playing for Jean-Marc Guillou's ASEC Mimosas in the Ivory Coast  Enzi hizo Yaya Toure akisukuma kabumbu pekupeku Ivory Coast katika klabu ya Asec Memosac
Yaya Toure aliwasili Ubelgiji akiwa hana chochote bali kipaji chake. Hiyo ndio kumbukumbu waliyokuwa nayo juu ya Toure pale Beveren: hakuwa hata na pea za viatu vya kuchezea soka.
Early days: Toure (circled) in the African-dominated team at BeverenYaya Toure Alipotua Ubelgiji
Nyingine ni kwamba hakuwa na tabia ya kuamka mapema asubuhi; alikuwa anakula kama farasi na kunywa kama samaki, soda ya fanta na sio pombe.
Yaya Toure alitua Beveren, mji mdogo uliopo magharibi mwa Antwerp, akiwa tu ndio anafikisha miaka 18, akiwa amelelewa kwa kuongea lugha ya kifaransa katika mitaa ya Abidjan, Ivory Coast. Alikuwa na pesa kidogo sana, pair moja ya viatu na nguo chache.


Sheria nzuri za Ubelgiji zilikuwa na manufaa kwa Guilloi ambaye sasa kashayapatia maisha. Ada yoyote ya uhamisho kwa wachezaji watakaouzwa kutoka klabu hiyo - ilikuwa inagawanywa pasu kwa pasu. Guillou na Beveren.

Sheria nzuri za Ubelgiji zilikuwa na manufaa kwa Guilloi ambaye sasa kashayapatia maisha. Ada yoyote ya uhamisho kwa wachezaji watakaouzwa kutoka klabu hiyo - ilikuwa inagawanywa pasu kwa pasu. Guillou na Beveren.

Yaya Toure akiwa Arsenal
Mwaka 2003, kutokana na uhusiano uliopo kati ya Arsenal na Guillou pamoja Beveren Yaya Toure akapelekwa London kwa majaribio ya muda mfupi. Japokuwa sasa anafananishwa na Patrick Vieira - haikuwa hivyo mwanzoni.

Toure alicheza mechi ya pre-season dhidi ya Barnet lakini dimba la juu. Aidha Toure hakumshawishi au Wenger tayari alikuwa na mbadala wake, kijana kutoka Ivory Coast akarudi Ubelgiji. Wote wawili Wenger na Toure wameshasemakulikuwa na matatizo juu ya passport.
'Labda alikuwa bado hajakaa sawa,' alisema Martin Keown, ambaye bado alikuwa Arsenal kipindi hicho.

"Kulikuwa na attention kubwa sana juu yake kwa sababu alikuwa mdogo wake Kolo, lakini Yaya hakuwa na mwezi wa mazoezi wa pre-season kama wengine . Labda mwili wake bado haukuwa sawa.

"Lakini pamoja na yoteYaya aliacha gumzo. Yeye na kaka yake ni wakarimu na watu wazuri sana. Na wanapenda mpira - tumekuwa tukisikia kuhusu watoto wa mzee Neville walivyo, ndugu hawa wa Toure nao wapo hivyo hivyo."

Aliporudi Ubelgiji Toure hakukataa tamaa aliendeleza juhudi ya kujifunzana mazoezi na hata tabia zake hazikubadilika.
Ingawa katika mahojiano aliyoyafanya na Dailymail Toure anasema alifanya mambo mengi ya kijinga alipokuwa Beveren lakini hakuna mtu anakumbuka. lakini Danny Stuer mkufunzi wa mazoezi ya viungo anasema tofauti: "Yaya alikuwa mtu wa maadili, tofauti sana, muda wote mkimya na mtu anayependa kufanya kazi. Alikuwa anakuja gym na alikuwa proffessional tangu mwanzo - wengine wote hawakuwa hivyo - kwao gym ilikuwa mchezo mtu.

"Baada ya mechi Yaya hakuwa akitoka kwenda kunywa mabia kama wenzie. Alirudi nyumbani na kubaki kupumzika huku akiangalia TV, hasa soka na soka zaidi."

"Mwanzoni alikuwa akiishi na wenzie lakini wenzake walipokuwa wanatoka usiku na kurudi wamechelewahuanza kumsumbua. Hivyo mwishowe akaomba aishi peke yake, na klabu ikafanikisha hilo.

"Labda alienda kwenye party nyuma ya mgongo wangu kama wengine- lakini kwa kile ninachojua Yaya alikuwa tofauti"
Pale Beveren walikuwa wanajua wachezaji wa kiafrika walikuwa wakienda Liege au Brussels kwa ajili ya kupati.
Baada ya misimu miwili na nusu na mechi 70 akiwa na Beveren, Toure aliuzwa kwa fedha ya ubelgiji millioni 2.
Mahasimuwawili wa Ubelgiji, Anderlecht na Club Bruges, wote walikuwa wakimtaka Toure, lakini sio kwa bei hiyo. Hivyo akiwa na miaka 20, akahamia Ukraine kwenye timu ya daraja ya pili ya Donetsk, Metalurh. Haikuwa sehemu nzuri kwa mtu ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa star wa dunia, lakini Toure anasema uhamisho huo ulikuwa mzuri kwake. "Soka ni kazi; nilijifunza hivyo Ukraine."

Baada ya muda kidogo -akahamia Ugiriki na kujiunga na Olympiakos. Club Bruges inaweza kuwa ilikataa kulipa €2m lakini manager wao, mnorway Trond Sollied, ambaye alijiunga na Olympiakos akamsaini Toure na kushinda kombe la Ugiriki. "Niliona almasi, kitu fulani special kwake, alipokuwa pale Beveren," anasema Sollied. "Hakuwa na nguvu alizonazo sasa, au kufunga magoli mengi lakini alikuwa na kitu extra ndani ya timu.

"Kumpata na kumleta Ugiriki ilikuwa ni vizuri. Kimwili alikuwa amepevuka, alikuwa yupo vizuri kuliko alivyokuwa Ukraine. Tulijua hatutoweza kukaa nae sana. Alikuwa na uhakika sana kuhusu alivyo. Nafikiri kaka yake alimsaidia. Walikuwa wakibadilishana uzoefu."

Baada ya kombe la dunia la mwaka 2006, AS Monaco, timu ya zamani ya Wenger, ilimnunua Toure kwa ada ya £4million, ingawakulikuwa na kutokuelewana kidogo kule Donetsk kuhusu mkataba wake.

YAYA TOURE ALIPOKUWA BARCELONA.
Yaya Toure and Eidur Gudjohnsen (L-R) Eric Abidal, Bojan Krkic , Sergi Busquets, Giovanni Dos Santos, Lionel Messi, Yaya Toure and Eidur Gudjohnsen of FC Barcelona during a practice session at the UCLA campus on July 30, 2009 in Los Angeles, California.  FC Bracelona will play a friendly soccer match against the Los Angeles Galaxy on August 1, 2009, at the Rose Bowl in Pasadena, California.

Lakini baada ya msimu mmoja tu nchini Ufaransa, Barcelona wakamsaini. Yaya Toure akaenda Catalunya ambako alipata majina mengi kama vile "Colossus - yaaani sanamu kubwa sana la mtu", wengine wakamuita "Treni " lakini Pep Guardiola alimuelezea Yaya kama "Diesel Player" - inachukua muda muda mrefu kwenda anapopataka lakini hasimami. Huyu ndiyo Yaya Toure ambaye ama kwa hakika ndio kiungo bora kabisa katika msimu huu wa Premier League ambayo inaisha Jumapili huku mwenyewe akitimiza miaka 29 siku hiyo.Na ana hamu kubwa ya kurudi Barca kuchezea timu hiyo.

No comments:

Post a Comment