Beki wa Manchester united Rafael Da Silva, ameitwa kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa ya Brazil kumbadili Daniel Alves wa Barcelona ambae aliumia majuzi mazoezini akiwa na Klabu yake.
Brazil, chini ya Kocha Mano Menezes, inatarajiwa kucheza Mechi za kirafiki baadae Mwezi huu ikiwa ni maandalizi yao ya kushiriki Michuano ya London ya Olimpiki Mwezi Julai.
Uteuzi wa Rafael unafanya Brazil iwe na Wachezaji 18 wenye chini ya Miaka 23 ambao ndio wanaruhusiwa kucheza Olimpiki na ni watatu tu wenye zaidi ya umri huo ndio wanatakiwa wawemo kwenye Kikosi rasmi cha Wachezaji 23.
Wachezaji ambao wana umri wa zaidi ya Miaka 23 walioitwa awali Kikosini ni Kipa Jefeerson na Mabeki Thiago Silva, David Luiz, Marcelo na Daniel Alves.
Shirikisho la Soka la Brazil, CBF, limesema Kocha Menezes atakuwepo Munich, Germany kushuhudia Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kati ya Bayern Munich na Chelsea na pia ndio Mji ambao Kikosi cha Brazil kitajumuika kwa ajili ya Mechi yao ya kirafiki na Denmark itakayochezwa Mei 26.
KIKOSI KAMILI
Makipa: Jefferson (Botafogo), Neto (Fiorentina), Rafael (Santos)
Mabeki: Rafael Da Silva (Manchester United), Marcelo (Real Madrid), Danilo, Alex Sandro (both Porto), Thiago Silva (AC Milan), David Luiz (Chelsea), Bruno Uvini (Tottenham Hotspur), Juan (Inter Milan)
Viungo: Casemiro, Lucas (both Sao Paulo), Sandro (Tottenham Hotspur), Romulo (Vasco da Gama), Paulo Henrique Ganso (Santos), Oscar (Internacional), Giuliano (Dnipropetrovsk)
Mafowadi: Alexandre Pato (AC Milan), Hulk (Porto), Leandro Damiao (Internacional), Neymar (Santos), Wellington Nem (Fluminense)
RATIBA MECHI ZA BRAZIL
Mei 26=Brazil v Denmark [Mjini Hamburg, Germany]
Mei 30=USA v Brazil [Washington, USA]
Juni 3=Brazil v Mexico [Dallas, USA]
Juni 9=Brazil v Argentina [New Jersey,USA]
No comments:
Post a Comment