BUKOBA SPORTS

Sunday, June 24, 2012

BALOTELLI: SIMWOGOPI MTU YEYOTE


Mario balotelli amewaambia wachezaji wenzake wa manchester city wanaokipiga katika timu ya taifa ya uingereza kwamba hamwogopi mtu yeyote wakati timu hizo zitakapokutana leo usiku katika pambano la kugombea kufuzu kwa nusu fainali ya Euro 2012 pambano litakalopigwa katika mji wa Kiev nchini Ukrane.

Balotelli ambaye anatarajiwa kuanza katika pambano la leo usiku amesema kwamba yeye na wachezaji wenzake wa italy wamepanga kuvuruga mipango ya england katika kuwania taji hilo la ulaya. Mchezaji huyo ambaye aliisaidia italy kushinda pambano lake na Ireland amesema anajisikia furaha kukutana na wachezaji wenzake wa mancity na kwamba anafikiri kwamba pambano la leo litakuwa zuri sana.

No comments:

Post a Comment