BUKOBA SPORTS

Thursday, June 7, 2012

COPA COCA-COLA: KUANZA KUCHEZWA JUNI 24 KWENYE UWANJA WA KARUME DAR ES SALAAM!

COPA COCA-COLA: Kuanza Juni 24 kuchezwa Dar na Pwani
Ile michuano ya Vijana COPA Coca Cola itaanza kuchezwa Juni 24 kwenye Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kwa pambano la ufunguzi kati ya Kigoma na Lindi litakalochezwa Uwanja wa Kumbkumbu ya Karume Jijini Dar es Salaam.
Habari hizi za Mashindano hayo yanayoshirikisha Timu za Mikoa 28 ya kimpira kwa ajili ya Vijana wa chini ya Miaka 17 na ambao walizaliwa kuanzia Januari 1 Mwaka 1996 zimetolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, TFF.
Hivi sasa, Makocha 35 wa Timu za Copa Coca-Cola kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani wako kwenye Kozi ya Shirikisho la Kimataifa la Soka, FIFA, inayoendeshwa na Wakufunzi Ulric Mathiot wa FIFA kutoka Seychelles na wa Shirikisho la Soka Afrika, CAF, Sunday Kayuni wa Tanzania.
Mikoa 28 ya kimpira ya Tanzania itashiriki katika mashindano hayo na imegawanywa katika Makundi manne ya Timu 7 kila moja.
Timu mbili toka Kila Kundi zitasonga Robo Fainali na Fainali ya michuano hii itafanyika Julai 15.
MAKUNDI
Kundi A: Arusha, Ilala, Kigoma, Kusini Pemba, Lindi, Rukwa na Ruvuma.
Kundi B:  Iringa, Kaskazini Pemba, Manyara, Mjini Magharibi, Morogoro, Mwanza na Tanga.
Kundi C: Dodoma, Kaskazini Unguja, Kinondoni, Mara, Mbeya, Mtwara na Temeke.
Kundi D: Kagera, Kilimanjaro, Kusini Unguja, Pwani, Shinyanga, Singida na Tabora.
Viwanja vitakavyotumika katika Mashindano haya ambapo mechi zitakuwa zikichezwa Asubuhi (saa 2.30) na Jioni (saa 10.00) ni Uwanja wa Karume na Tanganyika Packers (Kawe) kwa Dar es Salaam.
Viwanja vya Mkoa wa Pwani ni Tamco na Nyumbu.
Ile michuano ya Vijana COPA Coca Cola itaanza kuchezwa Juni 24 kwenye Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kwa pambano la ufunguzi kati ya Kigoma na Lindi litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Jijini Dar es Salaam.
Habari hizi za Mashindano hayo yanayoshirikisha Timu za Mikoa 28 ya kimpira kwa ajili ya Vijana wa chini ya Miaka 17 na ambao walizaliwa kuanzia Januari 1 Mwaka 1996 zimetolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, TFF.
Hivi sasa, Makocha 35 wa Timu za Copa Coca-Cola kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani wako kwenye Kozi ya Shirikisho la Kimataifa la Soka, FIFA, inayoendeshwa na Wakufunzi Ulric Mathiot wa FIFA kutoka Seychelles na wa Shirikisho la Soka Afrika, CAF, Sunday Kayuni wa Tanzania.
Mikoa 28 ya kimpira ya Tanzania itashiriki katika mashindano hayo na imegawanywa katika Makundi manne ya Timu 7 kila moja.
Timu mbili toka Kila Kundi zitasonga Robo Fainali na Fainali ya michuano hii itafanyika Julai 15.
 
MAKUNDI
Kundi A: Arusha, Ilala, Kigoma, Kusini Pemba, Lindi, Rukwa na Ruvuma. 
Kundi B: Iringa, Kaskazini Pemba, Manyara, Mjini Magharibi, Morogoro, Mwanza na Tanga. 
Kundi C: Dodoma, Kaskazini Unguja, Kinondoni, Mara, Mbeya, Mtwara na Temeke.
Kundi D: Kagera, Kilimanjaro, Kusini Unguja, Pwani, Shinyanga, Singida na Tabora.
Viwanja vitakavyotumika katika Mashindano haya ambapo mechi zitakuwa zikichezwa Asubuhi (saa 2.30) na Jioni (saa 10.00) ni Uwanja wa Karume na Tanganyika Packers (Kawe) kwa Dar es Salaam. 
Viwanja vya Mkoa wa Pwani ni Tamco na Nyumbu.

No comments:

Post a Comment