Rooney alikosa mechi mbili za hatua ya makundi kwa sababu alikuwa akitumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyokuwa ameipata katika mechi ya kuwania kufuzu kucheza mashindano hayo ya Euro 2012. Mashambuliaji huyo mashuhuri wa England alipata kadi hiyo nyekundu katika mechi dhidi ya Montenegro, lakini amemaliza adhabu yake na anatarajiwa kuikabili Ukraine huko mjini Donetsk. "Wayne kurudi uwanjani ni faida kubwa kwetu na atatuongezea nguvu katika safu ya ushambuliaji, nilisema kabla hatujaanza kushiriki mashindano haya kwamba jambo la msingi ni kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi mbili za mwanzo kabla Wayne hajarudi uwanjani, na kweli tumepata pointi nne ambazo siyo mbaya,"alisema Gerrard. "Tunaamini Wayne atatusaidia na ataongeza morali wa wachezaji, mashabiki watakuwa na nguvu zaidi ya kutushangilia kila mtu England atakuwa na furaha kuona mshambuliaji nyota wa England, Wayne atakapokuwa amerudi uwanjani,"alisema Gerrard. Alisema,"Wayne alikuwa hafurahii hata kidogo kukosa mechi zetu mbili tulizocheza, Wayne anapenda soka, anatamani awepo uwanjani." Akimzungumzia Wayne Rooney kocha wa England, Roy Hodgson alisema,"Wayne ni mchezaji mwenye ubora wa hali ya juu, naweza kusema ni mchezaji soka wa kidunia." Alisema,"unakuwa na bahati ukiwa kocha wa timu ya taifa halafu una wachezaji kama Wayne katika kikosi chako, nilikuwa sifurahii kumkosa Wayne, lakini hivi sasa amerudi naamini na matokeo ya mechi zetu zijazo yatakuwa tofauti." "Mimi sina wasiwasi kuhusu Wayne ila naamini ataleta mabadiliko makubwa katikia kikosi changu na Wayne hakumbushwi wajibu wake kwa sababu anajua anachotakiwa kufanya,"alisema Hodgson. Hodgson alisema,"unajua katika kundi letu kila timu ina wachezaji wenye ubora wa kidunia ila sisi tulikuwa tuna mkosa mmoja, ninasema hivyo kwa sababu Sweden inaye Zlatan Ibrahimovic , Ukraine inaye Andriy Shevchenko, Ufaransa inao Franck Ribery na Samir Nasri, sisi tulikuwa na Gerrard tu, lakini hivi sasa tutakuwa na Wayne pia. |
Tuesday, June 19, 2012
EURO 2012: ENGLAND WAFURAHIA MCHEZO WAO NA UKRAINE KWA MSHAMBULIAJI WAO ROONEY KUCHEZA!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment