Timu ya England ya soka imeondolewa katika mashindano ya Euro 2012, baada ya kufungwa na Italia usiku wa Jumapili katika robo fainali, kwa kufungwa magoli 4-2 ya penalti mjini Kiev, Ukraine, kufuatia muda wa kawaida na dakika 30 zaidi kumalizika kwa timu hizo mbili kutofungana.
Italia sasa itapambana na Ujerumani katika mechi ya nusu fainali.Alessandro Diamanti alifunga bao la kuamua mshindi katika mikwaju hiyo ya penalti, baada ya Ashley Young na Ashley Cole kukosa kufunga mabao kupitia mikwaju waliyopiga.
Vijana wa meneja Roy Hodgson ilikuwa wazi walilemewa katika mchezo mzima, lakini ni hali ya imani na uvumilivu iliwafanya kuwa na matazamio ya kuishinda Italia.
Italia iliweza kugonga mwamba, na bao la Antonio Nocerino lilikataliwa baada ya mwamuzi kusema aliotea mpira.
Kadri mechi ilivyoendelea, ndivyo wachezaji wa England nao walionekana wachovu, na ikielekea walitazamia bahati zaidi kuliko kujitahidi kuimarisha kiwango cha mchezo wao, na penalti kwao bila shaka ikawa sio za kutegemewa tena.
Baada ya mechi, nahodha Steven Gerrard alisema: "Wachezaji
walicheza kadri ya uwezo wao wote. Nilidhani tungelipata bahati katika mikwaju ya penalti, lakini mambo hayakuwa hivyo.
Roman Abramovich alikuwepo akifuatilia mtanange huo wa jana usiku
mwenyekiti wa FA David Bernstein akiwa karibu na Rais wa UEFA Michel Platini kwenye Mtanange
MIKWAJU: WALIOFUNGA NA KUKOSA
| ITALY | ENGLAND |
|---|---|
| Balotelli - SCORED Montolivo - MISSED Pirlo - SCORED Nocerino - SCORED DIAMANTI - SCORED | Gerrard - SCORED Rooney - SCORED Young - MISSED Cole - MISSED |
VIKOSI
England: Hart, Johnson, Terry, Lescott, Cole, Milner, Gerrard, Parker, Young, Rooney, Welbeck
Akiba: Green, Kelly, Walcott, Henderson, Carroll, Baines, Jones, Jagielka, Downing, Oxlade-Chamberlain, Defoe, Butland.
Italy: Buffon, Abate, Barzagli, Bonucci, Balzaretti, Pirlo, Marchisio, De Rossi, Montolivo, Balotelli, Cassano
Akiba: Sirigu, Maggio, Chiellini, Ogbonna, Thiago Motta, Di Natale, Giaccherini, Borini, Giovinco, Diamanti, Nocerino, De Sanctis.
Refa: Pedro Proenca (Portugal)
RATIBA/MATOKEO
ROBO FAINALI
[Mechi zote Saa 3 Dak 45 Usiku]
Alhamisi Juni 21
RF1: Warsaw, Poland: Czech Republic 0 Portugal 1
Ijumaa Juni 22
RF2: Gdansk, Poland: Germany 4 Greece 2
Jumamosi Juni 23
RF3: Donetsk, Ukraine: Spain 2 France 0
Jumapili Juni 24
RF4: Kiev, Ukraine: England 0 Italy 0 [Penati 2-4]
NUSU FAINALI
[Mechi zote Saa 3 Dak 45 Usiku]
Jumatano Juni 27
NF1: Donetsk, Ukraine: Portugal v Spain
Alhamisi Juni 28
NF2: Warsaw, Poland: Germany v Italy
FAINALI
Jumapili Julai 1
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Kiev, Ukraine: Portugal/Spain v German/Italy
No comments:
Post a Comment