BUKOBA SPORTS

Sunday, June 24, 2012

EURO 2012 LIVE: NANI KUSIMAMISHWA LEO KATI YA ENGLAND V ITALY


BAADA ya kushinda mechi mbili mfululizo, England na kuongoza Kundi D, England leo ikiongozwa na Wayne Rooney itasaka tiketi ya kucheza Nusu Fainali ya Euro 2012 kwa kumenyana na Italia.
Winga Ashley Young anaelekea kuwa fiti baada ya kuwa majeruhi, hivyo kocha Roy Hodgson anatarajiwa kuanza na kikosi kile kile kilichocheza mechi iliyopita mjini Donetsk, huku Theo Walcott na Alex Oxlade-Chamberlain wakiwa na matumaini ya kuchukua nafasi ya James Milner katika wingi ya kulia.

Nyuma, beki Glen Johnson anaendelea na matibabu kwa dawa za kuua sumu kwenye kidole cha mguu, lakini hiyo haitamfanya akose mechi ya leo.
Kwa upande mwingine, kocha wa Italia, Cesare Prandelli anatarajiwa kuendelea na mfumo wake wa 4-3-1-2 uliompa ushindi dhidi ya Ireland kuliko mfumo wa 3-5-2 uliomfanya akatoa sare na Hispania na Croatia.
Pamoja na hayo, atamuacha benchi beki wa kati Giorgio Chiellini, ambaye ni majeruhi aliyeumia katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Ireland na sasa anaweza kukosa mechi zote zilizobaki kama The Azzurri itasonga mbele.
Thiago Motta naye yuko shakani kucheza, kutokana na maumivu ya misuli na nafasi yake inaweza kuchukuliwa na Alessandro Diamanti au Riccardo Montolivo.
Formidable: Italy have performed above expectations so far in the Euro 2012 tournamentkikosi cha Italy kikifanya mazoezi jana
Mbele, Mario Balotelli anaweza kuanza ili apambane na wachezaji wenzake wa Manchester City, akichukua nafasi ya Antonio Di Natale kucheza pamoja na Antonio Cassano, baada ya kufunga bao katika mechi iliyopita.
Hakuna mchezaji anayetumikia adhabu, lakini Ashley Cole, Steven Gerrard, Milner, Oxlade-Chamberlain, and Young (wote England) na Balotelli, Federico Balzaretti, Leonardo Bonucci, Daniele De Rossi, Christian Maggio, Montolivo, Thiago Motta and Gianluigi Buffon (wote Italia) wamebakiza kadi moja moja za njano ili kukosa Nusu Fainali.

No comments:

Post a Comment