France nao jana usiku walipigwa bao 2-0 na Sweden waliokuwa tayari wameaga Mashindano lakini wamesonga kama Washindi wa Pili na watacheza na Mabingwa Watetezi Spain kwenye Robo Fainali.
Ukraine 0 England 1
Wayne Rooney, aliyekuwa akicheza Mechi yake ya kwanza ya EURO 2012 baada ya kifungo cha Mechi mbili, ndie aliefunga bao pekee na la ushindi kwa England.
Lakini, utata ulizuka baada ya Ukraine kufunga bao ambalo Waamuzi hawakuliona na marudio yalionyesha mpira uliokolewa na John Terry ukiwa umevuka mstari.
John Terry akijaribu kuokoa goli ambalo pia lilileta utata baada ya waamuzi kutoliona goli hilo jana usiku.
wote tumeliona hilo goli kwenye nyavu.....
computer inaonesha mpira uliingia ndani ya nyavu!!!
VIKOSI:
ENGLAND: Hart, Johnson, Terry, Lescott, Cole, Milner, Gerrard,
Parker, Young, Rooney, Welbeck.
Akiba: Green, Kelly, Walcott, Henderson, Carroll, Baines, Jones, Jagielka, Downing, Oxlade-Chamberlain, Defoe, Butland.
UKRAINE: Pyatov, Gusev, Khacheridi, Selin, Rakitskiy,
Yarmolenko, Tymoschuk, Konoplianka, Garmash, Devic, Milevskiy.
Akiba: Koval, Kucher, Shevchenko, Aliev, Voronin, Shevchuk,
Rotan, Seleznyov, Mykhalyk, Nazarenko, Butko, Goryainov.
Refa: Viktor Kassai (Hungary)
France 0 Sweden 2
Sweden, ambao walikuwa tayari nje ya Mashindano, wameipiga France bao 2-0 kwa bao za Kipindi cha Pili za Zlatan Ibrahimovich na Larsson na kuwafanya France wacheze Robo Fainali na Mabingwa Watetezi wa Ulaya, Spain, ambao pia ni Mabingwa wa Dunia.
VIKOSI
SWEDEN: Isaksson, Granqvist, Mellberg, Jonas Olsson, Martin Olsson, Svensson, Kallstrom, Larsson, Ibrahimovic, Bajrami, Toivonen
Akiba: Wiland, Lustig, Elm, Elmander, Hysen, Antonsson, Wernbloom, Safari, Holmen, Wilhelmsson, Rosenberg, Hansson.
FRANCE: Lloris, Debuchy, Rami, Mexes, Clichy, Nasri, Diarra, M'Vila, Ben Arfa, Ribery, Benzema
Akiba: Mandanda, Evra, Cabaye, Valbuena, Giroud, Matuidi, Reveillere, Menez, Malouda, Martin, Koscielny, Carrasso.
Refa: Pedro Proenca (Portugal)
RATIBA
ROBO FAINALI
[Mechi zote Saa 3 Dak 45 Usiku]
Alhamisi Juni 21
RF1: Warsaw, Poland: Czech Republic v Portugal
Ijumaa Juni 22
RF2: Gdansk, Poland: Germany v Greece
Jumamosi Juni 23
RF3: Donetsk, Ukraine: Spain v France
Jumapili Juni 24
RF4: Kiev, Ukraine: England v Italy
NUSU FAINALI
[Mechi zote Saa 3 Dak 45 Usiku]
Jumatano Juni 27
NF1: Donetsk, Ukraine: Czech Republic/Portugal v Spain/France
Alhamisi Juni 28
NF2: Warsaw, Poland: Germany/Greece v England/Italy
FAINALI
Jumapili Julai 1
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Kiev, Ukraine: NF1 v NF2
No comments:
Post a Comment