Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa yeye si Meneja tena wa Spurs, Redknapp, Miaka 65, amedai: “Ni ngumu, ile ilikuwa Timu ambayo ingeweza kuwa Bingwa wa Ligi Kuu! Nlikuwa natamani niwe kwenye Timu hiyo ya Mabingwa!”
Aliongeza: “Alex Ferguson ana Miaka 70 na bado ni Meneja Bora Duniani. Nipo fiti! Napenda Soka! Nafaa kwa kazi yeyote! Sijafikia mwisho wangu! ”
Redknapp, aliedumu Miaka minne hapo Spurs na kubakisha Mwaka mmoja kwenye Mkataba wake na Tottenham, ameelezea kuwa Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy alitaka mwanzo mpya baada ya kuiona Klabu yake ikiteleza na Arsenal kuipiku toka nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England Msimu ulioisha majuzi.
Tottenham ilikuwa kwenye kinyang’anyiro cha Ubingwa Msimu huu lakini ikamaliza nafasi ya 4, nyuma ya Manchester City, Manchester United na Arsenal, na ingeweza kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI kama si Chelsea kutwaa Ubingwa wa Ulaya na hivyo Msimu ujao kutakiwa kucheza CHAMPIONZ LIGI kutetea Taji lao na Tottenham kubwagwa kwenye EUROPA LIGI.
Msimu wa Mwaka 2009/10, chini ya Redknapp, Spurs ilimaliza nafasi ya 4 na kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI na kutolewa kwenye Robo Fainali.
Redknapp amefafanua: “Inasikitisha kwa njia nyingine lakini hii ni Soka. Watu wanaomiliki Klabu wanatoa maamuzi yao. Ni haki yao. Sina kinyongo. Sipati wasiwasi kuwa nini kingetokea. Nimeacha Kikosi imara, ni ngumu kwani Timu hiyo ingeweza kutwaa Ubingwa. Nilitamani nigekuwa mmoja kwenye hilo!”
No comments:
Post a Comment