BUKOBA SPORTS

Sunday, June 24, 2012

JOLEON LESCOTT: NITAMDHIBITI BALOTELLI

Beki mahiri wa timu ya taifa ya Uingereza Joleon Lescott amesema anatarajia kutakua na upinzani  mkali sana kati yake na mshambuliaji mtukutu wa timu ya taifa ya Italia Super Mario Balotelli kwenye mchezo wa robo fainali wa michuano ya EURO utakaopigwa baadae jioni hii kwenye jiji la Kiev nchini Ukraine. Mara nyingi wachezaji hao wakiwa katika mazoezi ya klabu yao ya Manchester City wamekua wakicheza kwa kukamiana sana, kiasi kwamba kufikia hata kuchezeana rafu. Lescott akizungumzia upinzani wake na Balotelli kwenye mazoezi alisema.http://m.gmgrd.co.uk/res/602.$plit/C_71_article_1581686_image_list_image_list_item_0_image.jpg?21%2F06%2F2012%2008%3A16%3A47%3A153
 “Kwenye mazoezi mara nyingi tunakua na upinzani mkubwa, ila huwa nafanikiwa kwa kiasi kikubwa kumdhibiti, lakini kwenye mechi ya mashindano kama ya leo kwenye hatua ngumu kama hii natarajia kupata upinzani mkali sana kutoka kwake. Ila naamini tukicheza pamoja kitimu tunaweza kuibuka na ushindi.”

No comments:

Post a Comment