BUKOBA SPORTS

Friday, June 15, 2012

BARCELONA YATHIBITISHA MENEJA WAO TITO VILANOVA KUSAINI MKATABA!


Leo, Barcelona imethibitisha kuwa Meneja wao mpya Tito Vilanova amesaini Mkataba wa Miaka miwili.
Mwezi Aprili ilitangazwa kuwa Vilanova ndie atamrithi Pep Guardiola ambae aliamua mwenyewe kuachia ngazi baada ya kuiongoza Barca kwa Miaka minne iliyokuwa na mafanikio makubwa.
 
Vilanova, Miaka 42, ndie alikuwa Msaidizi wa Guardiola kwenye Kipindi hicho.
Habari za Vilanova kusaini Mkataba zilithibitishwa pia kwenye Tovuti ya Barcelona ambayo ilitoa taarifa maalum.
 

No comments:

Post a Comment