BUKOBA SPORTS

Wednesday, June 27, 2012

MASHINDANO YA 126 YA WIMBLEDON YALIYOANZA RASMI JUMATATU

Li Na aliondolewa mapema katika French Open lakini anatazamiwa kufanya vyema katika mapambano ya Wimbledon
Mashindano ya tennis ya Wimbledon nchini Uingereza yameanza Jumatatu, na kati ya wachezaji mahiri wanaoshiriki ni pamoja na Novak Djokovic kutoka Jamhuri ya Serbia, Maria Sharapova ambaye ni raia wa Urusi na Roger Federer kutoka Uswisi.
Waingereza saba pia wanashiriki katika mashindano ya mwaka huu.
Kati ya wachezaji ambao mambo yameanza kuwaendea vyema Jumatatu ni Mchina Li Na, ambaye moja kwa moja ameingia raundi ya pili ya mashindano, kwa kumuondoa Ksenia Pervak wa Kazakhstan 6-3, 6-1.Mashabiki wakiwa nje ya uwanja wakiendelea kuangalizia mtanange kwenye Tv
Baada ya kuondolewa mapema katika mashindano ya French Open  katika raundi ya nne, Li Na inaelekea ameongeza juhudi za kufanya vyema katika mapambano ya Wimbledon.
Hata hivyo alionekana amemzidi nguvu Pervak, mwenye umri wa miaka 21, na alimuondoa haraka chini ya muda wa saa moja.
Sasa Li Na atakutana na Sorana Cirstea kutoka Romania, au Mfaransa Pauline Parmentier, katika raundi ya pili.
THE SCHEDULE
Mon, June 25: Singles first round
Tues, June 26
: Singles first round
Wed, June 27
: Singles second round; doubles events begin
Thurs, June 28
: Singles second round
Fri, June 29
: Singles third round
Sat, June 30
: Singles third round; junior events begin
Mon, July 2
: Singles fourth round
Tues, July 3
: Women’s quarter-finals
Wed, July 4
: Men’s quarter-finals
Thurs, July 5
: Women’s semi-finals
Fri, July 6
: Men’s semi-finals
Sat, July 7
: Women’s Final; men’s doubles final; mixed doubles final
Sun, July 8
: Men’s Final; women’s doubles final

No comments:

Post a Comment