BUKOBA SPORTS

Friday, June 29, 2012

KAGAME CUP: YANGA KUANZA NA ATLETICO YA BURUNDI JULAI 14


Katibu mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye 

Mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) wataanza kutetea ubingwa wao Julai 14 mwaka huu dhidi ya Atletico ya Burundi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye ametangaza ratiba ya michuano hiyo leo (Juni 29 mwaka huu) katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Timu 11 zitashiriki katika michuano hiyo itakayoanza Julai 14 hadi 28 mwaka huu ambapo kwa siku zitachezwa mechi mbili (saa 8 mchana na saa 10 jioni) huku Tanzania Bara ikiwakilishwa na Yanga, Simba na Azam. Mechi ya kwanza siku ya ufunguzi (saa 8 mchana) itakuwa kati ya APR ya Rwanda na Wau Salaam ya Sudan Kusini.

Kundi A lina timu za Simba, URA ya Uganda, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Ports ya Djibouti. Azam, Mafunzo ya Zanzibar na Tusker ya Kenya ziko kundi B.


Yanga inaunda kundi C lenye timu za APR ya Rwanda, Wau Salaam ya Sudan Kusini na Atletico ya Burundi.

Timu nane zitaingia robo fainali itakayochezwa Julai 23 na 24 mwaka huu. Kundi A na C kila moja litatoa timu tatu kwenda robo fainali wakati B litatoa timu mbili.

El Merreikh ya Sudan, Red Sea ya Eritrea, Coffee ya Ethiopia na Elman ya Somalia hazitashiriki katika mashindano ya mwaka huu ambayo yanafanyika Tanzania Bara kwa mwaka wa tatu mfululizo kutokana na sababu mbalimbali.


Coffee haitashiriki kwa vile ligi ya Ethiopia inaanza Julai 14 mwaka huu wakati El Merreikh wikiend ya Julai 13-15 mwaka huu itakuwa na mechi ya michuano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Bingwa wa michuano hiyo atapata dola 30,000, makamu bingwa dola 20,000 na mshindi wa tatu dola 10,000. Michuano hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) na Televisheni ya SuperSport.
 
KAGAME CUP 2012 FIXTURE
Sat. 14th July   1  APR vs WAU SALAAM          Uwanja wa Taifa            2pm
                       2 YANGA vs ATLETICO           Uwanja wa Taifa            4pm
 
Sun. 15th July   3 AZAM vs MAFUNZO             Chamazi                         4pm
 
Mon. 16th July   4 VITA CLUB vs PORTS           Uwanja wa Taifa            2pm
                        5 SIMBA vs URA                     Uwanja wa Taifa            4pm
 
Tue. 17th July   6 ATLETICO vs APR                Uwanja wa Taifa            2pm
                       7 WAU SALAAM vs YANGA       Uwanja wa Taifa            4pm
 
Wed. 18th July  8 VITA CLUB vs URA               Uwanja wa Taifa            2pm
                        9 PORTS vs SIMBA                  Uwanja wa Taifa           4pm
 
Thu. 19th July   10 ATLETICO vs WAU SALAAM  Uwanja wa Taifa          2pm
                       11 MAFUNZO vs TUSKER          Uwanja wa Taifa          4pm
 
Fri. 20th July    12 PORTS vs URA                     Uwanja wa Taifa         2pm
                       13 YANGA vs APR                    Uwanja wa Taifa         4pm
 
Sat. 21st July   14 AZAM vs TUSKER                  Uwanja wa Taifa         2pm
                      15 SIMBA vs VITA CLUB             Uwanja wa Taifa         4pm
 
Sun. 22nd July  REST DAY
 
QUARTER FINALS
Mon. 23rd July   16 B2 vs C2
                        17 A1 vs C3
 
Tue. 24th July   18 C1 vs A2
                        19 B1 vs A3
 
Wed. 25th July     REST DAY
 
SEMI FINALS
Thu. 26th July    20 Winner 16 vs Winner 17
Thu. 26th July    21 Winner 18 vs Winner 19
 
Fri. 27th July      REST DAY
 
FINALS AND 3rd PLACE PLAY OFFS
Sat. 28th July  22 Loser 20 vs Loser 21
                     23 Winner 20 vs Winner 21

No comments:

Post a Comment