BUKOBA SPORTS

Friday, June 22, 2012

WENGER: DILI LA KUMNYAKUA OLIVIER GIROUD LIMEKAMILIKA ASILIMIA 90!!

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ametamka kuwa dili ya kumnunua Olivier Giroud imekamilika kwa Asilimia 90.
Giroud, Miaka 25, ni Straika wa Montellier aliepachika bao 25 Msimu uliokwisha juzi na kuisaidia Klabu yake kutwaa Ubingwa wa Ligue 1 huko Ufaransa.
Straika huyo, ambaye yuko kwenye Kikosi cha France kinachocheza EURO 2012, ataigharimu Arsenal Pauni Milioni 13 kumnunua.
Wenger, akiongea kama Mchambuzi wa Soka kwa ajili ya EURO 2012 kwenye Kituo cha TV cha France TF1, alisema: “Giroud hajacheza sana kwenye EURO 2012 lakini atakuwa Mchezaji wa Arsenal Msimu ujao, hii ni Asilimia 90 tayari. Nadhani ana kipaji na atajumuika vizuri katika staili yetu ya Uchezaji. Ni Mchezaji anaecheza kitimu na anajua kushirikiana vyema na wenzake.”
Akimzungumzia Straika wa Germany Lukas Podolski ambae tayari washamnunua kutoka FC Cologne, Wenger alisema: “Podolski amefanya kazi njema kwa Germany, anacheza kitimu. Wakati mwingine hucheza kwa tahadhari lakini alifunga bao muhimu dhidi ya Denmark kwenye Mechi yake ya 100 kwa Germany. Nimefurahi kwa nilichokiona.”
Inategemewa mara tu baada ya Dili ya Giroud kukamilika, Arsenal wataanza kuwaondoa Wachezaji wao ambao hawana namba wakiwemo Nicklas Bendtner, Marouane Chamakh, Carlos Vela na Denilson.
Pia, inaaminika Arsenal wapo mbioni kujaribu kumsajili Kiungo wa Rennes ya Ufaransa Yann M'Vila hasa baada ya Bayern Munich kuondoa nia yao ya kumchukua.

No comments:

Post a Comment