Kipingu ambaye ni mdau mkubwa wa michezo nchini, akiwa ni mmoja ya watu waliochangia upatikanaji wa vipaji vya wachezaji wengi kama Juma Kaseja, Boniface Pawasa na wengine wengi wakati akiwa mkuu wa wa shule ya Makongo, anatarajiwa kuchukua fomu ndani ya kipindi cha masaa 72 kutoka kutoka sasa.
Kwa maana hiyo sasa Kipingu atakuwa akichuana na mfanyabiashara maarufu ambaye ameshaidhamini Yanga Yusuph Manji ambaye nae tayari ameshachukua fomu rasmi ya kugombea ubosi wa klabu bingwa ya afrika mashariki na kati.
No comments:
Post a Comment