
Bendera ya Zanzibar Ikipepea Wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Dunia ya Nchi zisizo wanachama wa FIFA
Timu ya Taifa Zanzibar (Zanzibar Heroes)imeanza vizuri michuano ya Kombe la Dunia ya nchi zisizo wanachama wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni(Fifa) baada ya kuizabua timu ya Ratia mabao 6-0.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari Chama cha Soka Zanzibar(ZFA), Munir Zakaria mabao ya Zanzibar Heroes yalikwamishwa na winga Hamis Mcha aliyepiga 'hat trick' katika dakika za 33, 41 na 72.
Mabao mengine yalifungwa na kiungo Abdi Kasim 'Babi' katika dakika ya 51 na Amir Juma aliyekwamisha mawili katika dakika ya 88 na 90.
Zacharia alisema baada ya ushindi huo Zanzibar itashuka tena dimbani leo kwenye Uwanja wa Erbil kuvaana na Tamil Eelam likiwa ni pambano la kukamilisha hatua ya makundi.
No comments:
Post a Comment