Klabu ya soka ya Ac Milan ya nchini Italia wanajiandaa kutuma ofa kwenda klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza ili iweze kumchukua mshambuliaji wa majogoo hao wa jiji Andy Carroll kwa mkopo. Mkurugenzi wa Ac Milan Piersilvio Berlusconi wiki iliyopita alithibitisha jinsi anavyomkubali nyota huyo. Kwa pamoja bodi ya kurugenzi ya Ac Milan wanajiandaa kupeleka ofa nzuri kwa Liverpool ili kuweza kumchukua Carroll kwa mkopo wa mwaka mmoja, Kuna uwezekano mkubwa wa Carroll 23 kufurahia dili hili haswa pale kocha mpya wa klabu hiyo kusema kuwa yupo tayari kuchezesha kikosi hicho bila hata kuwa na mshambuliaji kama ilivyofanya timu ya taifa ya Hispania na kufanikiwa kuchukua kombe la EURO.
Carroll njiani kuelekea Ac Milan
No comments:
Post a Comment