KitChee walitangulia kupata bao baada ya kosa la Ignasi Miquel na Yago akafunga lakini mchezo mzuri wa Abou Diaby ulimfungulia Theo Walcott alienda kufunga bao la kusawazisha.
Lakini Dakika chache baadae Arsenal walijikuta wakipigwa bao la pili baada ya Kipa Wojciech Szczesny kuutema mpira wa Cheng Siu Waii na Dani Cancela akafunga.
Kipindi cha Pili Arsenal wakasawazisha tena kupitia Eisfeld baada ya kazi njema ya Gervinho.
Mechi inayofuata ya Arsenal ya kujipima nguvu ni Agosti 12 dhidi ya Cologne ya Ujerumani na Mechi hii itampa nafasi Mchezaji mpya Lukas Podolski kucheza dhidi ya Klabu yake ya zamani.
KIKOSI CHA ARSENAL KILICHOANZA
Szczesny, Eastmond, Miquel, Djourou, Gibbs, Diaby, Coquelin, Oxlade-Chamberlan, Walcott, Miyaichi, Chamakh
Theo Walcott akitupia kusawazisha mara baada ya kupata pasi safi ya Abou Diaby
kijana mdogo Ryo Miyaichiwa akichuana kuupata mpira
No comments:
Post a Comment