
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimetangaza kuanza kwa mgomo wa walimu kwa nchi nzima kuanzia Jully 30, mwaka huu baada ya asilimia 95.7 ya walimu kupiga kura za ndiyo kuridhia kuwepo kwa mgomo huo wa kutetea maslahi yao.
Rais wa CWT GRATIAN MUKOBA amesema kwa mujibu wa sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004, kifungu cha 80 Moja (d) hatua zote zimefuatwa katika kuandaa mgomo huo na kuwataka walimu wote washiriki kwa kukaa nyumbani mpaka hapo watakapopewa maelekezo mengine.
Akizungumza na Vombo vya habari Jijini Dar es Salaam, MUKOBA amesema mgomo huo ni halali na hauna uhusiano wowote na zoezi la Sensa ya watu na Makazi linalotarajia kufanyika usiku wa kuamkia tarehe 26, Agosti mwaka huu.
Kuhusiana na shauri la walimu kuwepo mahakamani MUKOBA amesema kitendo hicho hakiondoi utaratibu wa kuendelea na taratibu za mgomo kutokana na kutokuwepo kwa amri yoyote ya mahakama kusitisha mgomo huo.
No comments:
Post a Comment